Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Timothée 4.3
Bible en Swahili de l’est


1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;2 Timothée 3.1-3.9 2 Pierre 3.3 Jude 1.18 2 Thessaloniciens 2.3-2.12 1 Jean 4.6
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;Ephésiens 4.19 Romains 16.18 2 Pierre 2.1-2.3 2 Timothée 3.5 Jérémie 23.32
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.Romains 14.6 Hébreux 13.4 Genèse 9.3 1 Corinthiens 7.28 Colossiens 2.16
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;Romains 14.14 1 Timothée 4.3 Romains 14.20 Actes 21.25 1 Corinthiens 10.23
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.1 Timothée 4.3 1 Corinthiens 7.14 Luc 11.41 Genèse 1.25 Luc 4.4
6 Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.Colossiens 3.16 1 Timothée 1.10 Colossiens 4.7 Ephésiens 4.15-4.16 2 Pierre 3.1-3.2
7 Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.1 Timothée 1.4 2 Timothée 2.16 Tite 2.12 Hébreux 5.14 Tite 3.9
8 Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.Matthieu 6.33 1 Timothée 6.6 Job 5.19-5.26 Psaumes 84.11 Psaumes 145.19
9 Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa;1 Timothée 1.15
10 kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio.1 Timothée 2.4 1 Jean 4.14 1 Jean 2.2 1 Timothée 2.6 2 Corinthiens 11.23-11.27
11 Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.1 Timothée 6.2 1 Timothée 5.7 Tite 2.15 Tite 3.8 2 Timothée 4.2
12 Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.Tite 2.7 2 Timothée 2.22 1 Pierre 5.3 2 Timothée 2.15 1 Corinthiens 11.1
13 Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha.1 Corinthiens 14.26 1 Corinthiens 14.3 2 Timothée 2.15-2.17 1 Timothée 4.6 1 Timothée 4.16
14 Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.2 Timothée 1.6 1 Timothée 1.18 Actes 6.6 1 Thessaloniciens 5.19 Actes 13.3
15 Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.Matthieu 5.16 Psaumes 104.34 1 Timothée 4.6 Psaumes 119.99 1 Corinthiens 16.15
16 Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.Ezéchiel 33.7-33.9 Actes 20.26-20.28 Tite 2.7 Tite 1.9 Hébreux 12.15

Cette Bible est dans le domaine public.