1  Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 
2 Timothée 3.1-3.9  2 Pierre 3.3  Jude 1.18  2 Thessaloniciens 2.3-2.12  Jude 1.4  
 2  kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 
Ephésiens 4.19  Romains 16.18  Ephésiens 4.14  1 Rois 22.22  Romains 1.28  
 3  wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. 
Romains 14.6  Hébreux 13.4  Genèse 9.3  1 Corinthiens 7.28  Colossiens 2.16  
 4  Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 
Romains 14.20  Actes 21.25  Romains 14.14  1 Timothée 4.3  Actes 11.7-11.9  
 5  kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. 
1 Corinthiens 7.14  Luc 11.41  Genèse 1.25  Luc 4.4  Genèse 1.31  
 6  Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata. 
1 Timothée 1.10  Colossiens 4.7  Colossiens 3.16  1 Pierre 2.2  Psaumes 19.7  
 7  Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. 
1 Timothée 1.4  2 Timothée 2.16  Hébreux 5.14  Tite 3.9  Tite 2.12  
 8  Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye. 
Matthieu 6.33  1 Timothée 6.6  Psaumes 84.11  Psaumes 145.19  Marc 10.30  
 9  Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa; 
1 Timothée 1.15  
 10  kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio. 
1 Timothée 2.4  1 Jean 4.14  1 Jean 2.2  1 Timothée 2.6  2 Corinthiens 11.23-11.27  
 11  Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha. 
1 Timothée 6.2  1 Timothée 5.7  Tite 2.15  Tite 3.8  2 Timothée 4.2  
 12  Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. 
Tite 2.7  2 Timothée 2.22  1 Pierre 5.3  2 Timothée 2.15  1 Corinthiens 11.1  
 13  Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha. 
1 Timothée 3.14-3.15  Josué 1.8  1 Corinthiens 14.6  Romains 12.8  Psaumes 1.2-1.3  
 14  Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee. 
2 Timothée 1.6  1 Timothée 1.18  Actes 6.6  1 Thessaloniciens 5.19  1 Timothée 5.22  
 15  Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. 
Matthieu 5.16  Psaumes 63.6  Psaumes 143.5  Psaumes 19.14  Actes 6.4  
 16  Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia. 
Actes 20.26-20.28  Tite 2.7  Tite 1.9  Ezéchiel 33.7-33.9  2 Jean 1.8-1.9