Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Thessaloniciens 2.17
Bible en Swahili de l’est


1 Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,Marc 13.27 1 Thessaloniciens 4.14-4.17 Matthieu 24.31 Ephésiens 1.10 1 Thessaloniciens 3.13
2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.1 Jean 4.1-4.2 Marc 13.7 1 Corinthiens 1.8 Esaïe 26.3 1 Thessaloniciens 5.2
3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;Ephésiens 5.6 Daniel 7.25 1 Timothée 4.1-4.3 Matthieu 24.4-24.6 Jean 17.12
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.Ezéchiel 28.2 1 Corinthiens 8.5 Apocalypse 13.6-13.7 Esaïe 14.13-14.14 Ezéchiel 28.9
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?Matthieu 16.9 Marc 8.18 Jean 16.4 Galates 5.21 1 Thessaloniciens 2.11
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.2 Thessaloniciens 2.3 2 Thessaloniciens 2.8
7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.1 Jean 2.18 1 Jean 4.3 Apocalypse 17.7 Apocalypse 17.5 Colossiens 2.18-2.23
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;Esaïe 11.4 Apocalypse 19.15 2 Thessaloniciens 2.3 Daniel 7.10-7.11 Apocalypse 2.16
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;Matthieu 24.24 Apocalypse 18.23 Apocalypse 19.20 Deutéronome 13.1-13.2 Jean 8.44
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.Proverbes 1.7 1 Corinthiens 1.18 2 Corinthiens 4.2-4.3 Ephésiens 4.14 2 Corinthiens 2.17
11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;Romains 1.28 Ezéchiel 14.9 1 Thessaloniciens 2.3 Esaïe 66.4 Jean 12.39-12.43
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.Romains 1.32 Romains 2.8 Romains 12.9 Psaumes 11.5 Jean 3.19-3.21
13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;2 Timothée 1.9 1 Thessaloniciens 1.4 1 Thessaloniciens 5.9 Actes 13.48 2 Thessaloniciens 1.3
14 aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.1 Thessaloniciens 2.12 1 Thessaloniciens 1.5 1 Pierre 5.10 Romains 8.28-8.30 Jean 17.24
15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.1 Corinthiens 11.2 1 Corinthiens 16.13 2 Thessaloniciens 2.2 2 Thessaloniciens 3.6 Philippiens 4.1
16 Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,Jean 3.16 1 Thessaloniciens 3.11 1 Pierre 1.3-1.8 Ephésiens 5.25 Jean 4.14
17 awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.2 Thessaloniciens 3.3 1 Thessaloniciens 3.13 1 Thessaloniciens 3.2 2 Corinthiens 1.3-1.6 1 Pierre 5.10

Cette Bible est dans le domaine public.