La purification de la femme après l’accouchement
 1 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto mume, ndipo atakuwa yu najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi, ndivyo atakavyokuwa najisi.
Lévitique 15.19  Luc 2.22  Genèse 1.28  Lévitique 18.19  Genèse 3.16  
 3 Siku nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake.
Luc 2.21  Luc 1.59  Jean 7.22-7.23  Deutéronome 30.6  Colossiens 2.11  
 4 Na huyo mwanamke atakaa katika damu ya kutakata kwake siku thelathini na tatu; asiguse kitu kilicho kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu, hata siku hizo za kutakata kwake zitakapotimia.
Lévitique 15.25-15.28  Aggée 2.13  Luc 2.22-2.23  
 5 Lakini kwamba amezaa mtoto mke ndipo atakuwa najisi juma mbili, kama katika kutengwa kwake; naye atakaa katika damu ya kutakata kwake muda wa siku sitini na sita.
Genèse 3.13  Lévitique 12.4  1 Timothée 2.14-2.15  Lévitique 12.2  
 6 Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mwana, au kwa ajili ya binti, ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani;
Luc 2.22  Lévitique 14.22  Lévitique 5.6-5.10  2 Corinthiens 5.21  Nombres 6.10  
 7 na yeye atawasongeza mbele za Bwana, na kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atatakasika na jicho la damu yake. Hii ndiyo amri yake huyo azaaye, kwamba ni mtoto mume au mke.
Lévitique 4.26  Romains 3.23  Lévitique 4.20  Romains 3.26  Lévitique 1.4  
 8 Kama mali yake huyo mwanamke haimfikilii mwana-kondoo, hapo ndipo atakapochukua hua wawili, au makinda mawili ya njiwa; mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na wa pili kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.
Lévitique 5.7  Lévitique 4.26  Lévitique 1.14  Lévitique 14.22  Lévitique 15.14