Reproches contre les alliances politiques
 1  Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwivi huvunja nyumba za watu, na kundi la wanyang’anyi hushambulia nje. 
Osée 6.4  Osée 4.2  Esaïe 59.12  Michée 7.3-7.7  Jérémie 51.9  
 2  Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu. 
Psaumes 90.8  Jérémie 2.19  Jérémie 14.10  Hébreux 4.13  Jérémie 4.18  
 3  Humfurahisha mfalme kwa uovu wao, na wakuu wao kwa uongo wao. 
Romains 1.32  Michée 7.3  Jérémie 28.1-28.4  Jérémie 5.31  Michée 6.16  
 4  Hao wote ni wazinzi; wamekuwa kama tanuu iliyotiwa moto na mwokaji; huacha kuuchochea moto, tangu kuukanda unga hata umekwisha kutiwa chachu. 
Jérémie 9.2  Jacques 4.4  Jérémie 5.7-5.8  Osée 7.6-7.7  Osée 4.2  
 5  Sikukuu ya mfalme wetu, wakuu walijitapisha kwa ukali wa divai; alinyosha mkono wake pamoja na wenye mzaha. 
Esaïe 28.1  1 Rois 13.4  Psaumes 69.12  Esaïe 5.22-5.23  Proverbes 20.1  
 6  Maana wamefanya moyo wao kuwa tayari kama tanuu, wakati waoteapo; hasira yao hulala usiku kucha; asubuhi yawaka kama moto utoao miali. 
Michée 2.1  1 Samuel 19.11-19.15  Psaumes 21.9  Psaumes 10.8-10.9  Proverbes 4.16  
 7  Wote wamepata moto kama tanuu, nao hula makadhi wao; wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao aniitaye mimi. 
2 Rois 15.14  2 Rois 15.25  2 Rois 15.10  2 Rois 15.30  Esaïe 64.7  
 8  Efraimu ajichanganya na mataifa; Efraimu ni mkate usiogeuzwa. 
Psaumes 106.35  Osée 5.13  Sophonie 1.5  Néhémie 13.23-13.25  Osée 5.7  
 9  Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari. 
Osée 8.7  2 Rois 15.19  2 Rois 13.3-13.7  Proverbes 23.35  Esaïe 57.1  
 10  Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote. 
Osée 5.5  Esaïe 9.13  Amos 4.6-4.13  Proverbes 27.22  Romains 3.11  
 11  Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru. 
Osée 5.13  Osée 12.1  Osée 4.11  Osée 11.11  Osée 9.3  
 12  Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia. 
Ezéchiel 12.13  Deutéronome 28.15-28.68  Ecclésiaste 9.12  Job 19.6  Jérémie 16.16  
 13  Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu. 
Osée 9.12  Osée 11.12  Apocalypse 8.13  Deutéronome 15.15  Psaumes 106.10  
 14  Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi. 
Amos 2.8  Job 35.9-35.10  Michée 2.11  Zacharie 7.5  Juges 9.27  
 15  Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu. 
Nahum 1.9  2 Rois 13.5  2 Rois 14.25-14.27  Hébreux 12.5  Jérémie 17.9  
 16  Wao hurudi, lakini si kwake Aliye juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya jeuri ya ndimi zao; jambo hili litakuwa kwao sababu ya kuchekwa katika nchi ya Misri. 
Psaumes 78.57  Osée 9.3  Ezéchiel 23.32  Psaumes 73.9  Psaumes 12.4