Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 38.6
Bible en Swahili de l’est


1 Neno la Bwana likanijia, kusema, 2 Mwanadamu, kaza uso wako, umwelekee Gogu, wa nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali, ukatabiri juu yake,Ezéchiel 39.1 Genèse 10.2 Ezéchiel 27.13 Ezéchiel 38.3 Ezéchiel 6.2
3 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, na Mesheki, na Tubali;Ezéchiel 13.8 Ezéchiel 35.3 Ezéchiel 29.3 Ezéchiel 39.1-39.10
4 nami nitakugeuza na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;Ezéchiel 29.4 Ezéchiel 38.15 Daniel 11.40 Ezéchiel 39.2 2 Rois 19.28
5 Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;Ezéchiel 27.10 Genèse 10.6 Ezéchiel 30.5 Nahum 3.9 1 Chroniques 1.8
6 Gomeri, na vikosi vyake vyote; nyumba ya Togarma, pande za mwisho za kaskazini, na vikosi vyake vyote; naam, watu wengi pamoja nawe.Genèse 10.2-10.3 Ezéchiel 27.14 1 Chroniques 1.5-1.6 Daniel 11.40
7 Ujiweke tayari, naam, jiweke tayari, wewe na majeshi yako yote waliokukusanyikia, nawe uwe jemadari wao.Esaïe 8.9-8.10 Zacharie 14.2-14.3 2 Chroniques 25.8 Jérémie 46.3-46.5 Jérémie 46.14-46.16
8 Na baada ya siku nyingi utajiliwa; katika miaka ya mwisho, utaingia nchi iliyorudishiwa hali yake ya kwanza, baada ya kupigwa kwa upanga, iliyokusanywa toka kabila nyingi za watu, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa salama salimini wote pia.Esaïe 24.22 Ezéchiel 38.16 Ezéchiel 34.13 Ezéchiel 36.1-36.8 Jérémie 23.6
9 Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe.Esaïe 28.2 Jérémie 4.13 Joël 2.2 Esaïe 25.4 Ezéchiel 38.16
10 Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya;Psaumes 36.4 Michée 2.1 Actes 5.3 1 Corinthiens 4.5 Esaïe 10.7
11 nawe utasema, Nitapanda juu niiendee nchi yenye vijiji visivyo na maboma; nitawaendea watu wanaostarehe, wanaokaa salama, wote wakikaa pasipo kuta, ambao hawana makomeo wala malango;Zacharie 2.4-2.5 Proverbes 1.11-1.16 Juges 18.7 Jérémie 49.31-49.32 Romains 3.15
12 ili kuteka mateka, na kuwinda mawindo; uugeuze mkono wako juu ya mahali palipoharibika, ambapo sasa panakaliwa na watu, na juu ya watu waliokusanyika toka mataifa, waliopata ng’ombe na mali, wakaao katikati ya dunia.Ezéchiel 38.8 Ezéchiel 29.19 Esaïe 10.6 Jérémie 30.16 Zacharie 1.17
13 Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wana-simba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng’ombe na mali, kuteka mateka mengi sana?Ezéchiel 27.15 Ezéchiel 27.12 Ezéchiel 27.20 Ezéchiel 27.22-27.23 Ezéchiel 32.2
14 Basi, mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile watu wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari?Ezéchiel 38.8 Zacharie 2.5 Ezéchiel 38.11 Zacharie 2.8 Jérémie 23.6
15 Nawe utakuja kutoka mahali pako, kutoka pande za mwisho za kaskazini, wewe, na watu wa kabila nyingi pamoja nawe, wote wamepanda farasi, kusanyiko kubwa, na jeshi kuu;Ezéchiel 39.2 Ezéchiel 38.6 Sophonie 3.8 Apocalypse 16.16 Ezéchiel 38.4
16 nawe utapanda juu uwajilie watu wangu, Israeli, kama wingu kuifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.Ezéchiel 39.21 Ezéchiel 38.23 Michée 4.1 Ezéchiel 36.23 1 Timothée 4.1
17 Bwana MUNGU asema hivi; Je! Wewe ndiwe niliyemnena zamani za kale, kwa vinywa vya watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri siku zile kwa muda wa miaka mingi, ya kwamba nitakuleta upigane nao?Joël 3.9-3.14 Esaïe 63.1-63.6 Esaïe 66.15-66.16 Esaïe 34.1-34.6 Esaïe 27.1
18 Itakuwa katika siku hiyo, Gogu atakapokuja kupigana na nchi ya Israeli, asema Bwana MUNGU, ghadhabu yangu itapanda katika mianzi ya pua yangu.Hébreux 12.29 Nahum 1.2 Psaumes 18.7-18.8 Psaumes 89.46 Ezéchiel 36.5-36.6
19 Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;Aggée 2.6-2.7 Joël 3.16 Apocalypse 16.18 Ezéchiel 5.13 Ezéchiel 39.25
20 hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.Osée 4.3 Nahum 1.4-1.6 Jérémie 4.23-4.26 Apocalypse 6.12-6.13 2 Corinthiens 10.4
21 Nami nitaita upanga, uje juu yake katika milima yangu yote, asema Bwana MUNGU; nao upanga wa kila mtu utakuwa juu ya ndugu yake.2 Chroniques 20.23 1 Samuel 14.20 Juges 7.22 Aggée 2.22 Ezéchiel 14.17
22 Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.Psaumes 11.6 Jérémie 25.31 Apocalypse 16.21 Esaïe 28.17 Psaumes 18.12-18.14
23 Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.Ezéchiel 38.16 Psaumes 9.16 Ezéchiel 36.23 Ezéchiel 37.28 Apocalypse 19.1-19.6

Cette Bible est dans le domaine public.