Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 8.4
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana akaniambia, Ujipatie ubao mkubwa ukaandike juu yake kwa kalamu ya binadamu, Kwa Maher-shalal-hash-bazi;Esaïe 30.8 Jérémie 36.2 Apocalypse 13.18 Job 19.23-19.24 Esaïe 8.3
2 nami nitajipatia mashahidi waaminifu ili kuandika habari, yaani, Uria, kuhani, na Zekaria, mwana wa Yeberekia.2 Rois 16.10-16.11 Ruth 4.2 2 Rois 18.2 2 Corinthiens 13.1 2 Rois 16.15-16.16
3 Nami nikamwendea huyo nabii mke, naye akapata mimba, akazaa mtoto mwanamume. Kisha Bwana akaniambia, Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi.Juges 4.4 2 Rois 22.14 Osée 1.3-1.9 Esaïe 7.13-7.14
4 Kwa maana kabla mtoto huyo hajapata kujua kusema, Baba yangu, na Mama yangu, hazina za Dameski na mateka ya Samaria yatachukuliwa mbele ya mfalme wa Ashuru.Romains 9.11 2 Rois 16.9 Jonas 4.11 Esaïe 10.6-10.14 Esaïe 7.8-7.9
5 Kisha Bwana akasema nami mara ya pili, akaniambia,Esaïe 7.10
6 Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa yapitayo polepole, na kufurahi kwa ajili ya Resini na huyo mwana wa Remalia,Jean 9.7 Néhémie 3.15 Esaïe 7.1-7.2 Jérémie 2.18 Esaïe 7.6
7 basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote;Esaïe 17.12-17.13 Amos 8.8 Amos 9.5 Esaïe 7.17 Genèse 6.17
8 naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.Esaïe 7.14 Esaïe 30.28 Ezéchiel 17.3 Esaïe 36.1-36.22 Esaïe 10.28-10.32
9 Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande.Esaïe 17.12-17.13 Esaïe 14.5-14.6 1 Rois 20.11 Esaïe 7.1-7.2 Proverbes 11.21
10 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.Romains 8.31 Job 5.12 2 Samuel 15.31 Proverbes 21.30 Psaumes 46.7
11 Maana Bwana aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema,Ezéchiel 3.14 Ezéchiel 2.6-2.8 Jérémie 15.19 Actes 4.20 Psaumes 32.8
12 Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni fitina; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope.1 Pierre 3.14-3.15 Luc 21.9 Psaumes 53.5 2 Rois 16.5-16.7 Esaïe 30.1
13 Bwana wa majeshi ndiye mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu.Psaumes 76.7 Nombres 20.12-20.13 Malachie 2.5 Apocalypse 15.4 Nombres 27.14
14 Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.1 Pierre 2.8 Luc 2.34 Romains 9.32-9.33 Esaïe 28.16 Ezéchiel 11.16
15 Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.Matthieu 21.44 Esaïe 28.13 Romains 9.32 Matthieu 15.14 1 Corinthiens 1.23
16 Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu.Daniel 12.4 Esaïe 29.11-29.12 2 Rois 11.12 Deutéronome 4.45 Marc 10.10
17 Nami nitamngojea Bwana, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia.Esaïe 54.8 Habakuk 2.3 Deutéronome 32.20 Ezéchiel 39.23-39.24 Genèse 49.18
18 Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na Bwana tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa Bwana wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.Luc 2.34 Hébreux 2.13-2.14 Esaïe 7.3 Psaumes 9.11 Zacharie 8.3
19 Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?Esaïe 19.3 1 Samuel 28.8 2 Chroniques 33.6 Esaïe 29.4 Lévitique 20.6
20 Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.Esaïe 30.8-30.11 2 Pierre 1.19 Michée 3.6 Jean 5.39 Jean 5.46-5.47
21 Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;Esaïe 9.20 Jérémie 14.18 Deutéronome 28.33-28.34 Exode 22.28 Jérémie 52.6
22 nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapana changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.Esaïe 5.30 Sophonie 1.14-1.15 Jérémie 13.16 Jérémie 23.12 Matthieu 24.29

Cette Bible est dans le domaine public.