Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 57.5
Bible en Swahili de l’est


1 Mwenye haki hupotea, wala hakuna atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya.2 Rois 22.20 Psaumes 12.1 Esaïe 42.25 2 Chroniques 34.28 Esaïe 47.7
2 Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake.Apocalypse 14.13 Luc 2.29 Luc 16.22 2 Chroniques 16.14 Ezéchiel 32.25
3 Lakini ninyi karibuni hapa, enyi wana wa mwanamke mchawi, uzao wa mzinzi na kahaba.Matthieu 16.4 Apocalypse 17.1-17.5 Esaïe 45.20 Matthieu 23.33 Matthieu 3.7
4 Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani? Mmepanua vinywa vyenu, na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo;Esaïe 1.4 Psaumes 35.21 Psaumes 22.7 Osée 10.9 Esaïe 30.9
5 ninyi mnaowasha tamaa zenu kati ya mialoni, chini ya kila mti wenye majani mabichi; ninyi mnaoua watoto mabondeni, chini ya mianya ya majabali?Ezéchiel 16.20 2 Rois 16.3-16.4 Esaïe 1.29 Jérémie 2.20 Jérémie 3.13
6 Sehemu yako i katika makokoto ya bonde; hayo ndiyo kura yako; umeyamwagia hayo sadaka ya kinywaji, umeyatolea sadaka ya unga; je! Niwe radhi na mambo hayo?Jérémie 3.9 Jérémie 7.18 Habakuk 2.19 Esaïe 65.11 Ezéchiel 20.39
7 Umeweka kitanda chako juu ya mlima mrefu ulioinuka sana; ukaenda huko ili kutoa dhabihu.Ezéchiel 16.16 Ezéchiel 23.41 Ezéchiel 23.17 Jérémie 3.6 Ezéchiel 16.25
8 Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona.Ezéchiel 23.2-23.20 Ezéchiel 8.8-8.12 Ezéchiel 16.32 Ezéchiel 16.25-16.28 Ezéchiel 23.41
9 Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hata kuzimu.Ezéchiel 23.16 Osée 7.11 Esaïe 30.1-30.6 Osée 12.1 2 Rois 16.7-16.11
10 Ulikuwa umechoka kwa ajili ya urefu wa njia yako; lakini hukusema, Hapana matumaini; ulipata kuhuishwa nguvu zako; kwa sababu hiyo hukuugua.Jérémie 2.25 Jérémie 18.12 Habakuk 2.13 Jérémie 3.3 Jérémie 44.17-44.18
11 Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata ukasema uongo, wala hukunikumbuka mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu zamani, hata huniogopi?Proverbes 29.25 Psaumes 50.21 Jérémie 2.32 Esaïe 51.12-51.13 Jérémie 3.21
12 Mimi nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa.Michée 3.2-3.4 Esaïe 1.11-1.15 Matthieu 23.13 Esaïe 29.15 Esaïe 59.6-59.8
13 Utakapolia, na wakuponye hao uliowakusanya; lakini upepo utawachukua; uvuvio tu utawachukulia mbali; lakini yeye anayenitumaini ataimiliki nchi, na kuurithi mlima wangu mtakatifu.Psaumes 37.9 Esaïe 11.9 Psaumes 37.3 Esaïe 65.25 Esaïe 56.7
14 Naye atasema, Tutieni, tutieni, Itengenezeni njia, Kiondoeni kila kikwazacho Katika njia ya watu wangu.Esaïe 62.10 Luc 3.5-3.6 1 Corinthiens 8.13 Romains 14.13 Esaïe 40.3
15 Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.Psaumes 34.18 Psaumes 138.6 Exode 15.11 Daniel 4.34 Esaïe 66.1-66.2
16 Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya.Michée 7.18 Psaumes 85.5 Psaumes 78.38-78.39 Psaumes 103.9-103.16 Jérémie 10.24
17 Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake naliona hasira, nikampiga; nalificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.Esaïe 56.11 Jérémie 6.13 Esaïe 5.8-5.9 Jérémie 8.10 Esaïe 8.17
18 Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia.Osée 14.4-14.8 Jérémie 3.22 Jérémie 33.6 Jérémie 13.17 Apocalypse 7.17
19 Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema Bwana; nami nitamponya.Hébreux 13.15 Actes 2.39 Ephésiens 2.14-2.17 Luc 2.14 Esaïe 6.7
20 Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka.Job 18.5-18.14 Esaïe 3.11 Proverbes 4.16-4.17 Jude 1.12 Job 20.11-20.29
21 Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu.Esaïe 48.22 Romains 3.16-3.17 Esaïe 3.11 Esaïe 59.8 2 Rois 9.22

Cette Bible est dans le domaine public.