Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 61.5
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. 2 Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. 3 Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. 4 Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako 5 Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako. 6 Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. 7 Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi. 8 Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.

Cette Bible est dans le domaine public.