Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 60.11
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena.Psaumes 44.9 Psaumes 80.3 Psaumes 60.10 2 Samuel 10.16 2 Samuel 8.3
2 Umeitetemesha nchi na kuipasua, Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.2 Chroniques 7.14 Esaïe 30.26 Habakuk 3.10 Job 9.6 Esaïe 5.25
3 Umewaonyesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.Esaïe 51.22 Psaumes 71.20 Esaïe 51.17 Jérémie 25.15 Psaumes 75.8
4 Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.Psaumes 20.5 Esaïe 11.12 Cantique 2.4 Psaumes 45.4 Esaïe 59.14-59.15
5 Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie.Psaumes 17.7 Psaumes 108.6-108.13 Psaumes 60.12 Exode 15.6 Esaïe 41.10
6 Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi.Genèse 12.6 Josué 13.27 Psaumes 89.35 Josué 1.6 Amos 4.2
7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,Genèse 49.10 Deutéronome 33.17 Josué 13.31 1 Chroniques 12.37 1 Chroniques 12.19
8 Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita.2 Samuel 8.1-8.2 2 Samuel 8.14 2 Samuel 5.17-5.25 Genèse 25.23 1 Chroniques 18.13
9 Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?2 Samuel 12.26-12.31 1 Chroniques 11.17-11.19 1 Chroniques 11.6 Juges 1.12 Juges 1.24-1.25
10 Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?Psaumes 108.11 Josué 7.12 Psaumes 60.1 1 Chroniques 10.1-10.14 Deutéronome 20.4
11 Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai.Psaumes 146.3 Psaumes 62.1 Psaumes 108.12 Psaumes 124.1-124.3 Esaïe 31.3
12 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.Psaumes 44.5 Esaïe 63.3 Malachie 4.3 Nombres 24.18-24.19 Psaumes 118.16

Cette Bible est dans le domaine public.