Consécration et règne du divin roi
 1  Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili? 
Psaumes 46.6  Psaumes 21.11  Apocalypse 17.14  Psaumes 83.4-83.8  Actes 5.33  
 2  Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya Bwana, Na juu ya masihi wake. 
Jean 1.41  Matthieu 27.1  Luc 23.11-23.12  Psaumes 45.7  Apocalypse 17.12-17.14  
 3  Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao. 
Jérémie 5.5  Luc 19.14  1 Pierre 2.7-2.8  Luc 19.27  
 4  Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. 
Psaumes 59.8  Psaumes 37.13  Esaïe 40.22  Psaumes 11.4  Proverbes 1.26  
 5  Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake. 
Esaïe 11.4  Psaumes 110.5-110.6  Luc 19.27  Matthieu 23.33-23.36  Psaumes 50.16-50.22  
 6  Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu. 
Psaumes 45.6  Psaumes 48.1-48.2  Matthieu 28.18  Apocalypse 14.1  Esaïe 9.6-9.7  
 7  Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. 
Actes 13.33  Matthieu 3.17  Hébreux 5.5  Hébreux 1.5-1.6  Jean 3.16  
 8  Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako. 
Psaumes 22.27  Daniel 7.13  Psaumes 72.8  Jean 17.4-17.5  Psaumes 89.27  
 9  Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi. 
Apocalypse 12.5  Apocalypse 2.26-2.27  Psaumes 89.23  Esaïe 30.14  Apocalypse 19.15  
 10  Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe. 
Osée 14.9  Esaïe 52.15  Jérémie 6.8  Psaumes 72.10-72.11  Esaïe 49.23  
 11  Mtumikieni Bwana kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka. 
Philippiens 2.12  Hébreux 12.28-12.29  Hébreux 12.25  Psaumes 89.7  Psaumes 119.119-119.120  
 12  Shikeni yaliyo bora asije akafanya hasira, Nanyi mkapotea njiani,Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi,Heri wote wanaomkimbilia. 
Apocalypse 6.16-6.17  Jean 5.23  Romains 9.33  Esaïe 30.18  Jérémie 17.7