Prière pour la délivrance
 1  Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako. 
Psaumes 71.2  1 Jean 1.9  Psaumes 140.6  Psaumes 31.1  2 Samuel 7.25  
 2  Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki. 
Ecclésiaste 7.20  Job 25.4  Psaumes 130.3  Romains 3.20  Job 14.3  
 3  Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani. 
Psaumes 88.4-88.6  Psaumes 7.1-7.2  Psaumes 7.5  Psaumes 31.12-31.13  Psaumes 35.4  
 4  Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka. 
Psaumes 77.3  Psaumes 142.3  Job 6.27  Luc 22.44  Psaumes 124.4  
 5  Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. 
Psaumes 77.5-77.6  1 Samuel 17.45-17.50  Psaumes 77.10-77.12  Michée 6.5  1 Samuel 17.34-17.37  
 6  Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. 
Psaumes 63.1  Job 11.13  Psaumes 88.9  Psaumes 42.1-42.2  Psaumes 84.2  
 7  Ee Bwana, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni 
Psaumes 69.17  Psaumes 27.9  Psaumes 28.1  Esaïe 57.16  Psaumes 69.3  
 8  Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu. 
Psaumes 46.5  Psaumes 25.4-25.5  Esaïe 48.17  Esaïe 30.21  Psaumes 86.4  
 9  Ee Bwana, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche. 
Proverbes 18.10  Psaumes 61.3-61.4  Psaumes 59.1  Psaumes 142.5  Hébreux 6.18  
 10  Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, 
Néhémie 9.20  Psaumes 25.4-25.5  Psaumes 119.12  Hébreux 13.21  Psaumes 23.3  
 11  Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni; 
Psaumes 31.1  Psaumes 119.25  Psaumes 71.2  Psaumes 37.39-37.40  Psaumes 25.17  
 12  Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako. 
Psaumes 116.16  Psaumes 54.5  Psaumes 55.23  1 Samuel 26.10  Psaumes 52.5