Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 129.8
Bible en Swahili de l’est


1 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa, 2 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza. 3 Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao. 4 Bwana ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki. 5 Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni. 6 Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea. 7 Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake. 8 Wala hawasemi wapitao, Amani ya Bwana ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la Bwana.

Cette Bible est dans le domaine public.