Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 108.5
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Nitaimba, nitaimba zaburi, Naam, kwa utukufu wangu.Psaumes 57.7-57.11 Psaumes 71.15 Exode 15.1 Psaumes 145.21-146.2 Psaumes 145.1-145.2
2 Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.Psaumes 103.22 Psaumes 92.1-92.4 Psaumes 57.8 Psaumes 33.2 Psaumes 81.2
3 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.Psaumes 22.22 Psaumes 22.27 Psaumes 117.1 Sophonie 3.14 Sophonie 3.20
4 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni.Psaumes 36.5 Ephésiens 2.4-2.7 Michée 7.18-7.20 Psaumes 103.11 Esaïe 55.9
5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.Psaumes 57.5 Psaumes 57.11 1 Chroniques 29.10-29.13 Matthieu 6.9-6.10 Esaïe 6.3
6 Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, uniitikie.Psaumes 60.5-60.12 2 Samuel 12.25 Colossiens 3.12 Jérémie 33.3 Exode 15.6
7 Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi.Psaumes 89.35-89.36 Josué 17.7 2 Samuel 7.20-7.29 2 Pierre 1.3-1.4 Psaumes 16.9-16.11
8 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,Genèse 49.10 Deutéronome 33.17 Josué 13.8-13.11 1 Samuel 28.4 Psaumes 122.5
9 Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita.2 Samuel 21.15-21.22 Jean 13.8 Ruth 4.7-4.8 2 Samuel 8.1-8.2 Jean 13.14
10 Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?Esaïe 63.1-63.6 Psaumes 20.6-20.8 Abdias 1.3-1.4 Jérémie 49.7-49.16 Psaumes 60.1
11 Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?Psaumes 44.9 1 Samuel 17.36 2 Chroniques 20.15 1 Samuel 17.26 Deutéronome 20.3-20.4
12 Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai.Psaumes 20.1-20.9 Esaïe 30.3-30.5 Esaïe 31.3 Jérémie 17.5-17.8 Esaïe 2.22
13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.Esaïe 63.3 Psaumes 60.12 Psaumes 144.1 Psaumes 18.42 Esaïe 25.10

Cette Bible est dans le domaine public.