Prière dans la détresse
 1  Ee Bwana, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie. 
Psaumes 61.2  Exode 2.23  Psaumes 18.6  Lamentations 3.44  Psaumes 55.1-55.5  
 2  Usinifiche uso wako siku ya shida yangu, Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi. 
Psaumes 69.17  Psaumes 27.9  Psaumes 71.2  1 Corinthiens 10.13  Psaumes 143.7  
 3  Maana siku zangu zinatoweka kama moshi, Na mifupa yangu inateketea kama kinga. 
Jacques 4.14  Lamentations 1.13  Job 30.30  Psaumes 37.20  Psaumes 31.10  
 4  Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu. 
Psaumes 37.2  Esaïe 40.7  Esdras 10.6  Actes 9.9  Psaumes 143.3-143.4  
 5  Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwangu Mifupa yangu imegandamana na nyama yangu. 
Job 19.20  Proverbes 17.22  Lamentations 4.8  Psaumes 6.8  Psaumes 38.8-38.10  
 6  Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani, Na kufanana na bundi wa mahameni. 
Sophonie 2.14  Esaïe 38.14  Job 30.29-30.30  Michée 1.8  Esaïe 34.11-34.15  
 7  Nakesha, tena nimekuwa kama shomoro Aliye peke yake juu ya nyumba. 
Psaumes 77.4  Psaumes 38.11  Psaumes 130.6  Marc 14.33-14.37  Deutéronome 28.66-28.67  
 8  Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu Huapa kwa kunitaja mimi. 
Actes 26.11  Luc 6.11  Psaumes 31.11-31.13  Psaumes 89.51  Psaumes 69.20  
 9  Maana nimekula majivu kama chakula, Na kukichanganya kinywaji changu na machozi. 
Psaumes 42.3  Psaumes 80.5  Michée 7.17  Esaïe 44.20  Michée 1.10  
 10  Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira yako; Maana umeniinua na kunitupilia mbali. 
Psaumes 38.3  Lamentations 1.18  Lamentations 5.16  Psaumes 39.11  Psaumes 73.18-73.20  
 11  Siku zangu zi kama kivuli kilichotandaa, Nami ninanyauka kama majani. 
Job 14.2  Psaumes 109.23  Psaumes 144.4  Psaumes 102.3-102.4  Psaumes 39.5-39.6  
 12  Bali Wewe, Bwana utaketi ukimiliki milele, Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi. 
Psaumes 135.13  Psaumes 9.7  Exode 3.15  Lamentations 5.19  Apocalypse 1.17-1.18  
 13  Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia. 
Galates 4.4  Psaumes 44.26  Esaïe 40.2  2 Pierre 3.8  2 Pierre 3.12  
 14  Maana watumishi wako wameyaridhia mawe yake, Na kuyaonea huruma mavumbi yake. 
Néhémie 4.2  Néhémie 2.17  Psaumes 137.5-137.6  Daniel 9.16  Néhémie 4.6  
 15  Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana, Na wafalme wote wa dunia utukufu wako; 
1 Rois 8.43  Psaumes 138.4  Psaumes 68.31-68.32  Esaïe 60.3-60.22  Esaïe 55.5  
 16  Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, Atakapoonekana katika utukufu wake, 
Esaïe 60.1-60.2  Psaumes 147.2  Esaïe 66.18  Jérémie 31.4  Esaïe 60.7  
 17  Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao. 
Néhémie 1.6  Psaumes 22.24  Jérémie 29.11-29.14  Daniel 9.3-9.21  Psaumes 9.18  
 18  Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo, Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana. 
Romains 15.4  1 Corinthiens 10.11  Psaumes 22.30-22.31  Esaïe 43.21  Psaumes 78.4-78.6  
 19  Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi, 
Deutéronome 26.15  Psaumes 14.2  Hébreux 9.23-9.24  2 Chroniques 16.9  Psaumes 33.13-33.14  
 20  Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa. 
Psaumes 79.11  Psaumes 146.7  Esaïe 61.1-61.3  Esaïe 14.17  Actes 12.6-12.11  
 21  Watu walitangaze jina la Bwana katika Sayuni, Na sifa zake katika Yerusalemu, 
Psaumes 22.22  1 Pierre 2.9  Ephésiens 3.21  Psaumes 9.13-9.14  Ephésiens 2.4-2.7  
 22  Pindi mataifa watapokusanyika pamoja, Falme nazo ili kumtumikia Bwana. 
Zacharie 8.20-8.23  Matthieu 24.14  Psaumes 72.8-72.11  Esaïe 49.22-49.23  Psaumes 22.27  
 23  Amezipunguza nguvu zangu njiani; Amezifupisha siku zangu. 
2 Timothée 3.1-3.17  Apocalypse 11.2-11.19  Apocalypse 12.13-12.17  1 Timothée 4.1-4.3  Job 21.21  
 24  Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu; Miaka yako ni tangu kizazi hata kizazi. 
Habakuk 1.12  Psaumes 39.13  Psaumes 102.12  Apocalypse 1.8  Psaumes 90.1-90.2  
 25  Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako. 
Genèse 1.1  Hébreux 1.10-1.12  Genèse 2.1  Job 38.4-38.7  Jérémie 32.17  
 26  Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu Naam, hizi zitachakaa kama nguo; Na kama mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika. 
Esaïe 34.4  Esaïe 51.6  Apocalypse 20.11  Matthieu 24.35  Romains 8.20  
 27  Lakini Wewe U Yeye yule; Na miaka yako haitakoma. 
Malachie 3.6  Jacques 1.17  Hébreux 13.8  Apocalypse 1.17-1.18  Jean 8.58  
 28  Wana wa watumishi wako watakaa, Na wazao wao wataimarishwa mbele zako. 
Psaumes 45.16-45.17  Psaumes 69.35-69.36  Esaïe 65.22  Esaïe 53.10  Psaumes 89.4