Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 35.4
Bible en Swahili de l’est


1 Tena Elihu akajibu na kusema, 2 Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako, Au je! Wasema, Haki yangu ni zaidi kuliko ya Mungu,Matthieu 12.36-12.37 Job 27.2-27.6 Job 16.17 Luc 19.22 Job 10.7
3 Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe? Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi?Job 34.9 Malachie 3.14 Job 9.21-9.22 Psaumes 73.13 Job 21.15
4 Mimi nitakujibu, Na hawa wenzio pamoja nawe.Job 34.8 Proverbes 13.20
5 Ziangalie mbingu ukaone; Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe.Job 22.12 Esaïe 55.9 Nahum 1.3 Esaïe 40.22-40.23 Job 37.16
6 Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?Proverbes 8.36 Jérémie 7.19 Proverbes 9.12
7 Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako?Job 22.2-22.3 Romains 11.35 Proverbes 9.12 Luc 17.10 Psaumes 16.2
8 Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu.Job 42.8 Ecclésiaste 9.18 Josué 22.20 Genèse 12.2 Genèse 19.29
9 Kwa sababu ya wingi wa jeuri wao hulia; Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu.Exode 2.23 Job 34.28 Néhémie 5.1-5.5 Job 40.9 Exode 3.9
10 Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku;Psaumes 42.8 Psaumes 149.5 Actes 16.25 Esaïe 51.13 Psaumes 77.6
11 Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani?Psaumes 94.12 Job 36.22 Genèse 1.26 Job 32.8 Genèse 2.7
12 Hulia huko, lakini hapana ajibuye, Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.Proverbes 1.28 Jean 9.31 Psaumes 123.3-123.4 Esaïe 14.14-14.17 Psaumes 73.6-73.8
13 Hakika Mungu hatasikia ubatili, Wala Mwenyezi hatauangalia.Proverbes 15.29 Esaïe 1.15 Jérémie 11.11 Jacques 4.3 Job 27.8-27.9
14 Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii, Hiyo daawa i mbele yake, nawe wamngojea!Job 9.11 Job 23.3 Job 23.8-23.10 Romains 8.33-8.34 Job 9.19
15 Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujilia katika hasira zake, Wala hauangalii sana unyeti;Psaumes 89.32 Job 13.15 Luc 1.20 Osée 11.8-11.9 Apocalypse 3.19
16 Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili; Huongeza maneno pasipo maarifa.Job 38.2 Job 34.35-34.37 Job 3.1 Job 33.2 Job 33.8-33.12

Cette Bible est dans le domaine public.