Descendance de David
 1   Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli; 
2 Samuel 3.2-3.5  Josué 15.56  2 Samuel 13.29  1 Samuel 27.3  2 Samuel 13.1  
 2  wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi; 
2 Samuel 13.1  1 Rois 2.24-2.25  2 Samuel 18.14  2 Samuel 13.20-13.28  1 Chroniques 2.23  
 3  wa tano, Shefatia, wa Abitali; wa sita, Ithreamu, kwa Egla, mkewe. 
2 Samuel 3.5  
 4  Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akamiliki miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akamiliki miaka thelathini na mitatu. 
2 Samuel 2.11  2 Samuel 5.4-5.5  1 Rois 2.11  1 Chroniques 29.27  2 Samuel 5.14-5.16  
 5  Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu; 
2 Samuel 11.3  2 Samuel 12.24-12.25  2 Samuel 5.14-5.16  1 Chroniques 14.4-14.7  Matthieu 1.6  
 6  na Ibhari, na Elishua, na Elipeleti; 
1 Chroniques 14.5  2 Samuel 5.15  1 Samuel 14.5  
 7  na Noga, na Nefegi, na Yafia; 
2 Samuel 5.15-5.16  
 8  na Elishama, na Eliada, na Elifeleti, watu kenda. 
1 Chroniques 14.7  2 Samuel 5.14-5.16  
 9  Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wana wa masuria; na Tamari alikuwa umbu lao. 
2 Samuel 5.13  2 Samuel 13.1-13.20  
 10  Na mwanawe Sulemani alikuwa Rehoboamu; na mwanawe huyo alikuwa Abiya; na mwanawe huyo ni Asa; na mwanawe huyo ni Yehoshafati; 
1 Rois 11.43  1 Rois 15.24  2 Chroniques 17.1  1 Rois 15.8  1 Rois 14.31-15.1  
 11  na mwanawe huyo ni Yehoramu; na mwanawe huyo ni Ahazia; na mwanawe huyo ni Yoashi; 
2 Rois 8.24  2 Chroniques 21.17  2 Rois 11.21  2 Chroniques 21.1  2 Rois 8.16  
 12  na mwanawe huyo ni Amazia; na mwanawe huyo ni Uzia; na mwanawe huyo ni Yothamu; 
2 Rois 14.21  2 Rois 14.1  2 Chroniques 25.1  2 Rois 15.30  2 Chroniques 26.1  
 13  na mwanawe huyo ni Ahazi; na mwanawe huyo ni Hezekia; na mwanawe huyo ni Manase; 
2 Chroniques 33.1  2 Chroniques 29.1  2 Rois 18.1  2 Rois 16.1  2 Rois 16.20  
 14  na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia. 
2 Rois 23.30  2 Rois 21.19  2 Chroniques 34.1  2 Chroniques 36.1  2 Rois 23.34  
 15  Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu. 
2 Rois 23.34  
 16  Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia. 
Matthieu 1.11  2 Rois 24.6  2 Rois 24.17  Jérémie 22.24  2 Rois 24.8  
 17  Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli, 
Esdras 3.2  Esdras 5.2  Matthieu 1.12  Esdras 3.8  
 18  na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia.  
19  Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa umbu lao; 
Esdras 2.2  Aggée 2.2  Esdras 3.2  Zacharie 4.6-4.9  Aggée 2.4  
 20  na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano.  
21  Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania. 
Néhémie 10.22  
 22  Na wana wa Shekania ni hawa; Shemaya, na wana wa Shemaya; Hatushi, na Igali, na Baria, na Nearia, na Shafati, watu sita. 
Esdras 8.2  
 23  Na wana wa Nearia; Elioenai, na Hezekia, na Azrikamu, watu watatu.  
24  Na wana wa Elioenai; Hodavia, na Eliashibu, na Pelaya, na Akubu, na Yohana, na Delaya, na Anani, watu saba.