Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 44.34
Bible en Swahili de l’est


Mise à l’épreuve des frères de Joseph

1 Akamwamuru yule msimamizi wa nyumba yake akisema, Jaza magunia ya watu hawa chakula kwa kadiri wawezavyo kuchukua, utie na fedha ya kila mtu kinywani mwa gunia lake.
Genèse 42.25 Genèse 43.16 Genèse 43.19 Esaïe 3.1 Genèse 43.2
2 Na kikombe changu, kikombe kile cha fedha, ukitie kinywani mwa gunia la yule mdogo pamoja na fedha ya nafaka yake. Akafanya kama vile alivyomwambia Yusufu.
Deutéronome 8.16 Genèse 42.15-42.16 Deutéronome 13.3 Genèse 43.32 2 Corinthiens 8.8
3 Asubuhi kulipopambazuka, hao watu wakapewa ruhusa, wao na punda zao.
4 Na walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema?
Psaumes 35.12 Jean 10.32 Psaumes 109.5 Proverbes 17.13 Deutéronome 2.16
5 Je! Kikombe hiki, sicho anyweacho bwana wangu? Naye hufanya uaguzi kwa hicho. Mmefanya vibaya kwa kufanya hivi.
Genèse 30.27 Genèse 44.15 2 Rois 21.6 Lévitique 19.26 1 Rois 20.33
6 Akawafuata, akawapata, na kuwaambia maneno hayo.
7 Wakamwambia, Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya?
Ecclésiaste 7.1 2 Rois 8.13 Genèse 34.25-34.31 Hébreux 13.18 Genèse 35.22
8 Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu?
Exode 20.15 Genèse 42.27 Jacques 2.10-2.11 Genèse 43.12 Genèse 42.21
9 Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu.
Genèse 31.32 Actes 25.11 Job 31.38-31.40 Genèse 43.18 Genèse 44.16
10 Akasema, Basi na iwe hivyo kama mlivyosema, Mtu atakayeonekana kuwa nacho atakuwa mtumwa wangu, na ninyi mtakuwa hamna hatia.
Genèse 44.33 Matthieu 18.24-18.25 Exode 22.3 Genèse 44.17
11 Wakafanya haraka, wakashusha kila mtu gunia lake, na kufungua kila mtu gunia lake.
12 Naye akatafuta, akaanza kwa mkubwa na kuisha kwa mdogo. Kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini.
Genèse 44.2 Genèse 42.36-42.38 Genèse 44.26-44.32 Genèse 43.33 Genèse 43.14
13 Wakararua nguo zao, wakaweka kila mtu mzigo wake juu ya punda wake, wakarudi mjini.
2 Samuel 1.11 Nombres 14.6 Genèse 37.29-37.34 2 Samuel 13.19 2 Samuel 1.2
14 Akaja Yuda na ndugu zake nyumbani kwa Yusufu, naye mwenyewe alikuwamo, nao wakamwangukia kifudifudi.
Genèse 43.25 Genèse 50.18 Philippiens 2.10-2.11 Genèse 37.7-37.10 Genèse 43.16
15 Yusufu akawaambia, Ni tendo gani hili mlilolitenda? Hamkujua ya kwamba mtu kama mimi naweza kufanya uaguzi?
Genèse 39.8 Genèse 3.13 Genèse 21.26 Exode 32.1 Genèse 44.4-44.5
16 Yuda akasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake.
Genèse 44.9 Daniel 9.7 Nombres 32.23 Esaïe 27.9 Matthieu 7.2
17 Akasema, Hasha! Nisifanye hivi; mtu ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake, ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Nanyi enendeni zenu kwa amani kwa baba yenu.
2 Samuel 23.3 Genèse 37.32-37.33 Psaumes 75.2 Genèse 26.29 Genèse 42.18
18 Ndipo Yuda akamkaribia, akasema, Tafadhali, bwana wangu, mtumwa wako na aseme neno moja masikioni mwa bwana wangu, wala hasira yako isimwakie mtumwa wako, maana wewe u kama Farao.
Exode 32.22 Genèse 18.30 Genèse 41.40 Genèse 18.32 Genèse 41.44
19 Wewe, bwana wangu, ulituuliza watumwa wako, ukisema, Je! Mnaye baba, au ndugu?
Genèse 43.7 Genèse 42.7-42.10 Genèse 43.29
20 Tukakuambia wewe, bwana wangu, Tunaye baba, naye ni mzee, na mwana wa uzee wake ni mdogo, na nduguye amekufa; amebaki yeye peke yake wa katika tumbo la mamaye, na baba yake anampenda.
Genèse 37.3 Genèse 42.38 Genèse 42.36 Luc 7.12 Genèse 49.8
21 Ukatuambia watumwa wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie.
Genèse 42.15 Genèse 42.20 Jérémie 24.6 Genèse 43.29 Amos 9.4
22 Tukakuambia, bwana wangu, Kijana hawezi kumwacha babaye, maana akimwacha babaye, babaye atakufa.
Genèse 44.30 Genèse 42.38
23 Ukatuambia watumwa wako, Asiposhuka ndugu yenu mdogo pamoja nanyi, hamtaniona uso wangu tena
Genèse 43.3 Genèse 43.5 Genèse 42.15-42.20
24 Ikawa tulipokwenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamwarifu maneno yako, bwana wangu.
Genèse 42.29-42.34
25 Kisha baba yetu akanena, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo.
Genèse 43.2 Genèse 43.5
26 Tukasema, Hatuwezi kwenda; ndugu yetu mdogo akiwapo pamoja nasi, tutashuka, maana hatutaweza kuuona uso wa mtu huyo, ndugu yetu mdogo asipokuwa pamoja nasi.
Genèse 43.4-43.5 Luc 11.7
27 Mtumwa wako, baba yangu, akatuambia, Mnajua ya kuwa mke wangu alinizalia wana wawili;
Genèse 46.19 Genèse 29.28 Genèse 30.22-30.25 Genèse 35.16-35.18 Genèse 29.18-29.21
28 mmoja alitoka kwangu, nikasema, Bila shaka ameraruliwa, wala sikumwona tangu hapo.
Genèse 37.33 Genèse 37.13-37.14 Genèse 42.36 Genèse 42.38
29 Na mkiniondolea huyu naye, na madhara yakimpata, mtashusha mvi zangu na msiba kaburini.
Genèse 42.38 Genèse 44.31 Genèse 42.36 Psaumes 88.3-88.4 Deutéronome 31.17
30 Basi, nikienda kwa mtumwa wako, baba yangu, na huyu kijana hayupo pamoja nasi, iwapo roho yake imeshikamana na roho ya kijana;
1 Samuel 18.1 1 Samuel 25.29 Genèse 44.31 Genèse 44.17 Genèse 44.34
31 itakuwa atakapoona ya kwamba huyu kijana hayuko, atakufa; na watumwa wako watashusha mvi za mtumwa wako, baba yetu, kwa huzuni kaburini.
Genèse 44.29 Genèse 37.35 1 Samuel 4.17-4.18 Genèse 37.26-37.27 1 Thessaloniciens 4.13
32 Kwa maana mtumwa wako alijifanya mdhamini wa huyu kijana kwa baba yangu, nikisema, Nisipomrudisha kwako, nitakuwa na hatia kwa baba yangu sikuzote.
Genèse 43.8-43.9 Genèse 43.16
33 Basi, sasa nakusihi, uniache mimi mtumwa wako nikae badala ya huyu kijana kuwa mtumwa wa bwana wangu; na huyu kijana umwache aende pamoja na nduguze.
1 Jean 3.16 Hébreux 7.22 Exode 32.32 Romains 9.3 Romains 5.7-5.10
34 Kwa maana nitawezaje kumwendea baba yangu, na huyu kijana hayuko pamoja nami? Nisije nikayaona mabaya yatakayompata baba yangu.
Esther 8.6 Exode 18.8 Psaumes 116.3 Jérémie 52.10-52.11 Psaumes 119.143

Cette Bible est dans le domaine public.