Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 6.2
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako. 2 Bwana, unifadhili, maana ninanyauka; Bwana, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. 3 Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, Bwana, hata lini? 4 Bwana urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. 5 Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru? 6 Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu. 7 Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi. 8 Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa Bwana ameisikia sauti ya kilio changu. 9 Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu. 10 Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.

Cette Bible est dans le domaine public.