Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 3.1
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, 2 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. 3 Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. 4 Kwa sauti yangu namwita Bwana Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. 5 Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza. 6 Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote. 7 Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. 8 Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Cette Bible est dans le domaine public.