Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Deutéronome 20.19
Bible en Swahili de l’est


1 Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri.Psaumes 20.7 2 Chroniques 32.7-32.8 Deutéronome 31.8 Deutéronome 31.6 Esaïe 31.1
2 Na iwe, msongeapo mapiganoni, kuhani na akaribie na kusema na watu,Nombres 10.8-10.9 Nombres 31.6 2 Chroniques 13.12 1 Samuel 14.18 1 Samuel 30.7-30.8
3 awaambie, Sikizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche, wala msiteteme, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao;1 Timothée 6.12 Esaïe 8.12-8.13 Hébreux 13.6 Actes 18.9-18.10 Actes 27.24
4 kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.Deutéronome 1.30 Josué 23.10 Deutéronome 3.22 Josué 10.42 Romains 8.37
5 Na maakida na waseme na watu, na kuwaambia, Ni mtu gani aliye hapa aliyejenga nyumba mpya, wala hajaiweka wakfu? Aende akarudi nyumbani kwake, asije akafa mapiganoni, ikawekwa wakfu na mtu mwingine.Néhémie 12.27 Deutéronome 16.18 1 Samuel 17.18 Deutéronome 1.15 Nombres 31.48
6 Ni mtu gani aliye hapa aliyepanda shamba la mizabibu, wala hajatumia matunda yake? Aende akarudi nyumbani kwake asije akafa mapiganoni, yakatumiwa na mtu mwingine matunda yake.Lévitique 19.23-19.25 Jérémie 31.5 Esaïe 65.22 Sophonie 1.13 Deutéronome 28.1-28.30
7 Ni mtu gani aliye hapa aliyemposa mke wala hajaoa? Aende akarudi nyumbani kwake asije akafa mapiganoni, huyo mwanamke akaolewa na mume mwingine.Deutéronome 24.5 Deutéronome 28.30 Matthieu 1.18 2 Timothée 2.4 Luc 14.18-14.20
8 Tena maakida na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake.Juges 7.3 Deutéronome 1.28 Actes 15.37-15.38 Apocalypse 21.8 Apocalypse 3.16
9 Itakuwa hapo watakapokwisha wale maakida kusema na watu, na waweke majemadari wa majeshi juu ya watu. 10 Utakaposongea karibu ya mji kwenda kupigana juu yake, ndipo utakapowapigia ukelele wa amani.2 Corinthiens 5.18-6.1 Luc 10.5-10.6 2 Samuel 20.18-20.22 Zacharie 9.10 Esaïe 57.19
11 Itakuwa utakapokujibu kwa amani, na kukufungulia, ndipo watu wote watakaoonekana humo watakufanyia kazi ya shokoa, na kukutumikia.Josué 16.10 Lévitique 25.42-25.46 Josué 11.19-11.20 Juges 1.28 Juges 1.30-1.35
12 Na kwamba hautaki kufanya amani nawe, lakini utafanya vita juu yako, ndipo uuhusuru; 13 na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga;Psaumes 110.1 Psaumes 21.8-21.9 Nombres 31.7-31.9 2 Thessaloniciens 1.7-1.9 1 Rois 11.15-11.16
14 lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana, Mungu wako.Josué 8.2 Josué 22.8 Nombres 31.9 Nombres 31.35-31.54 Romains 8.37
15 Utaifanyia vivyo miji yote iliyo mbali sana nawe, isiyokuwa miji ya mataifa haya. 16 Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;Josué 11.14 Nombres 21.2-21.3 Nombres 33.52 Deutéronome 7.1-7.4 Josué 6.17-6.21
17 lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru Bwana, Mungu wako;Ezéchiel 38.21-38.23 Esaïe 34.5-34.6 Jérémie 48.10 Apocalypse 19.18 Deutéronome 7.1-7.2
18 wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya Bwana, Mungu wenu.Deutéronome 12.30-12.31 Exode 23.33 Psaumes 106.34-106.40 Exode 34.16 Deutéronome 7.4-7.5
19 Wewe utakapohusuru mji siku nyingi kwa kufanya vita juu yake, upate kuutwaa, usiangamize miti yake kwa kupeleka shoka juu yake, kwani utaweza kula matunda yake; wala usiiteme, kwa maana huo mti wa kondeni, je! Ni mtu, hata ukauzuie?Matthieu 21.19 Jean 15.2-15.8 Matthieu 3.10 Matthieu 7.15-7.20 Luc 13.7-13.9
20 Ila miti uijuayo si miti ya kuliwa iangamize, na kuitema; ukajenge maburuji juu ya mji ufanyao vita juu yako, hata uanguke.Esaïe 37.33 Jérémie 6.6 Ecclésiaste 9.14 Jérémie 33.4 2 Chroniques 26.15

Cette Bible est dans le domaine public.