Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ephésiens 1.8
Bible en Swahili de l’est


1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu.Colossiens 1.2 2 Corinthiens 1.1 1 Corinthiens 1.1-1.2 Romains 1.1 Galates 1.1
2 Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.Romains 1.7 Tite 1.4 2 Corinthiens 1.2 Galates 1.3
3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;2 Corinthiens 1.3 1 Pierre 1.3 Genèse 22.18 Jean 10.29-10.30 Ephésiens 2.6
4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.2 Timothée 1.9 Romains 8.28-8.30 Matthieu 25.34 Ephésiens 2.10 Jacques 2.5
5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.Ephésiens 1.11 Romains 8.29-8.30 1 Jean 3.1 Romains 8.14-8.17 Romains 8.23
6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.Ephésiens 1.12 Matthieu 3.17 Colossiens 1.13 Ephésiens 1.14 Esaïe 43.21
7 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.Romains 3.24 Colossiens 1.14 Ephésiens 3.16 Romains 2.4 Ephésiens 2.7
8 Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi;Colossiens 2.3 Esaïe 52.13 Jude 1.25 Apocalypse 5.12 1 Corinthiens 2.7
9 akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo.Colossiens 1.26-1.28 Romains 8.28 Ephésiens 1.11 Romains 16.25-16.27 Ephésiens 3.3-3.9
10 Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;Colossiens 1.20 Galates 4.4 Daniel 2.44 Philippiens 2.9-2.10 Marc 1.15
11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.Romains 8.28 1 Pierre 1.4 Ephésiens 3.11 Ephésiens 1.14 Hébreux 6.17
12 Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.Ephésiens 1.6 2 Thessaloniciens 2.13 Matthieu 12.18-12.21 Ephésiens 1.13-1.14 Esaïe 11.10
13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.Ephésiens 4.30 2 Corinthiens 1.22 Colossiens 1.4-1.6 Actes 2.33 1 Thessaloniciens 2.13
14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.2 Corinthiens 1.22 Ephésiens 4.30 2 Corinthiens 5.5 Galates 4.6 Romains 8.23
15 Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,Philémon 1.5 Colossiens 1.3-1.4 1 Timothée 1.5 2 Thessaloniciens 1.3 Psaumes 16.3
16 siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu,Romains 1.8-1.9 1 Thessaloniciens 5.17 Colossiens 1.9 Colossiens 1.3 Genèse 40.14
17 Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;Esaïe 11.2 Proverbes 2.5 2 Pierre 1.3 Jacques 3.17-3.18 Colossiens 1.9-1.10
18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;Actes 26.18 2 Corinthiens 4.6 Ephésiens 4.4 Ephésiens 1.7 Ephésiens 5.8
19 na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;Colossiens 2.12 Philippiens 2.13 2 Corinthiens 4.7 Ephésiens 3.7 Colossiens 1.29
20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;Marc 16.19 Matthieu 28.18 Actes 2.24-2.36 Hébreux 10.12 Hébreux 1.3
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;Colossiens 2.10 Colossiens 1.15-1.16 Hébreux 1.4 Colossiens 2.15 Philippiens 2.9-2.11
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambaloColossiens 1.18 Colossiens 2.10 Colossiens 2.19 Psaumes 8.6-8.8 1 Corinthiens 11.3
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.Colossiens 1.24 Ephésiens 4.12 Colossiens 1.18-1.19 1 Corinthiens 12.12-12.27 Colossiens 3.11

Cette Bible est dans le domaine public.