Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Zacharie 5.2
Bible en Swahili de l’est


1 Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la chuo lirukalo.Apocalypse 10.2 Apocalypse 5.1-5.14 Apocalypse 10.8-10.11 Jérémie 36.27-36.32 Esaïe 8.1
2 Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la chuo lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi.Zacharie 4.2 Genèse 6.11-6.13 Jérémie 1.11-1.14 Amos 7.8 Apocalypse 18.5
3 Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama ilivyo upande wa pili.Exode 20.15 Esaïe 24.6 Esaïe 43.28 Esaïe 48.1 Malachie 4.6
4 Nitaituma itokee, asema Bwana wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba yake yeye aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.Malachie 3.5 Lévitique 14.34-14.45 Proverbes 3.33 Habakuk 2.9-2.11 Job 18.15
5 Ndipo yule malaika aliyesema nami akatokea, akaniambia, Inua macho yako sasa, uone ni kitu gani kitokeacho.Zacharie 1.9 Zacharie 2.3 Zacharie 4.5 Zacharie 1.14 Zacharie 1.19
6 Nikasema, Ni kitu gani? Akasema, Kitu hiki ni efa itokeayo. Tena akasema, Huu ndio uovu wao katika nchi hii yote;Amos 8.5 Ezéchiel 44.10-44.11
7 na tazama, talanta ya risasi iliinuliwa; na tazama, mwanamke akaaye katikati ya hiyo efa.Esaïe 13.1 Jérémie 3.1-3.2 Esaïe 22.11 Ezéchiel 16.1-16.63 Esaïe 15.1
8 Akasema, Huyu ni Uovu; akamtupa chini katikati ya ile efa; akalitupa lile jiwe la risasi juu ya mdomo wa ile efa.Matthieu 23.32 Michée 6.11 Proverbes 5.22 Amos 9.1-9.4 Lamentations 1.14
9 Ndipo nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa kati ya dunia na mbingu.Osée 8.1 Matthieu 24.28 Deutéronome 28.49 Lévitique 11.19 Daniel 9.26-9.27
10 Ndipo nikamwambia yule malaika aliyesema nami, Hawa wanaipeleka wapi efa hii? 11 Akaniambia, Wanakwenda kumjengea nyumba katika nchi ya Shinari; tena ikiisha kutengenezwa, atawekwa huko mahali pake mwenyewe.Genèse 11.2 Daniel 1.2 Genèse 10.10 Genèse 14.1 Jérémie 29.28

Cette Bible est dans le domaine public.