Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Amos 2.1
Bible en Swahili de l’est


1 Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa;Sophonie 2.8-2.9 Esaïe 15.1-15.9 Jérémie 48.1-48.47 Ezéchiel 25.8-25.9 Esaïe 25.10
2 lakini nitapeleka moto juu ya Moabu, nao utayateketeza majumba ya Keriothi; na Moabu atakufa pamoja na mshindo, na kelele, na sauti ya tarumbeta;Jérémie 48.24 Jérémie 48.41 Amos 1.14 Esaïe 9.5 Jérémie 48.34
3 nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema Bwana.Jérémie 48.7 Nombres 24.17 Psaumes 2.10 Jérémie 48.25 Esaïe 40.23
4 Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana; wala hawakuzishika amri zake; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata;Ezéchiel 20.24 Ezéchiel 20.16 Ezéchiel 20.13 Esaïe 28.15 Osée 12.2
5 lakini nitapeleka moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu.Osée 8.14 Jérémie 17.27 Jérémie 21.10 Jérémie 37.8-37.10 Jérémie 39.8
6 Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Israeli, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu;Joël 3.3 Amos 5.11-5.12 Michée 3.2-3.3 2 Rois 18.12 Osée 13.2-13.3
7 nao hutwetea mavumbi yaliyo juu ya vichwa vya maskini, na kuipotosha njia ya mwenye upole; na mtu na baba yake humwendea mwanamke mmoja, hata kulitia unajisi jina langu takatifu;Amos 5.12 Michée 2.9 Ezéchiel 22.11 Michée 2.2 1 Corinthiens 5.1
8 nao hujilaza karibu na kila madhabahu juu ya nguo zilizowekwa rehani, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya watu waliotozwa fedha.Amos 6.6 Exode 22.26-22.27 Deutéronome 24.12-24.17 Ezéchiel 18.12 Osée 4.8
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.Malachie 4.1 Job 18.16 Exode 34.11 Genèse 15.16 Nombres 21.23-21.25
10 Pia naliwapandisha ninyi kutoka nchi ya Misri, nikawaongoza muda wa miaka arobaini jangwani, ili mpate kuimiliki nchi ya Mwamori.Deutéronome 2.7 Exode 12.51 Amos 3.1 Ezéchiel 20.10 Actes 13.18
11 Nami nikawainua watu miongoni mwa wana wenu wawe manabii, na katika vijana wenu wawe Wanadhiri; je! Sivyo hivyo, enyi wana wa Israeli? Asema Bwana.Nombres 6.2-6.3 Jérémie 7.25 Juges 13.4-13.7 Amos 7.12-7.13 2 Rois 17.13
12 Lakini mliwapa Wanadhiri mvinyo wanywe; mkawaamuru manabii, mkisema, Msifanye unabii.Amos 7.13 Michée 2.6 Esaïe 30.10 Amos 7.16 Jérémie 11.21
13 Tazameni, nitawalemea ninyi, Kama gari lilemeavyo lililojaa miganda.Esaïe 1.14 Ezéchiel 6.9 Esaïe 7.13 Ezéchiel 16.43 Malachie 2.17
14 Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio; Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake; Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;Jérémie 9.23 Ecclésiaste 9.11 Psaumes 33.16 Amos 9.1-9.3 Job 11.20
15 Wala apindaye upinde hatasimama; Wala aliye mwepesi wa miguu hataokoka; Wala apandaye farasi hatajiokoa nafsi yake;Psaumes 33.16-33.17 Ezéchiel 39.3
16 Naye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa Atakimbia uchi siku ile, asema Bwana.Jérémie 48.41 Juges 4.17 2 Rois 7.8-7.20 Marc 14.52

Cette Bible est dans le domaine public.