Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 56.3
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.Matthieu 3.2 Psaumes 85.9 Psaumes 50.23 Esaïe 26.7-26.8 Esaïe 1.16-1.19
2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote.Esaïe 58.13 Psaumes 112.1 Exode 31.13-31.16 Ezéchiel 20.20 Jérémie 17.21-17.22
3 Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu.Romains 15.9-15.12 1 Pierre 1.1 Matthieu 15.26-15.27 Esaïe 39.7 Actes 8.26-8.40
4 Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu;Esaïe 56.6 Esaïe 56.2 Josué 24.15 Jérémie 50.5 Psaumes 119.111
5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali.Esaïe 55.13 Apocalypse 3.12 Jean 1.12 1 Timothée 3.15 Esaïe 62.12
6 Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;Jacques 2.5 Apocalypse 1.10 Jacques 1.12 Actes 2.41 Esaïe 61.5
7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.Marc 11.17 Luc 19.46 Matthieu 21.13 Malachie 1.11 Esaïe 2.2-2.3
8 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.Jean 10.16 Esaïe 60.3-60.11 Ephésiens 2.14-2.16 Ephésiens 1.10 Jérémie 31.10
9 Enyi hayawani wote wa nyikani, njoni, Mle, enyi hayawani wote wa mwituni.Jérémie 12.9 Ezéchiel 39.17 Apocalypse 19.17-19.18 Esaïe 18.6 Ezéchiel 29.5
10 Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.Philippiens 3.2 Esaïe 29.10 Jérémie 14.13-14.14 Nahum 3.18 Ezéchiel 13.16
11 Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.Michée 3.11 Ezéchiel 13.19 Jérémie 22.17 Ecclésiaste 5.10 Esaïe 57.17
12 Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi.Psaumes 10.6 Esaïe 5.22 1 Corinthiens 15.32 Luc 12.19-12.20 Proverbes 23.35

Cette Bible est dans le domaine public.