Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 42.19
Bible en Swahili de l’est


1 Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.Philippiens 2.7 Esaïe 43.10 Esaïe 52.13 Luc 3.22 Matthieu 3.16-3.17
2 Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu.Matthieu 12.16-12.20 Zacharie 9.9 Luc 17.20 2 Timothée 2.24 Matthieu 11.29
3 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli.Matthieu 11.28 Esaïe 50.4 Esaïe 40.11 Psaumes 96.13 Psaumes 147.3
4 Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake.Esaïe 55.5 Genèse 49.10 Esaïe 53.2-53.12 Esaïe 60.9 Matthieu 12.21
5 Mungu Bwana anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake.Esaïe 45.18 Esaïe 45.12 Actes 17.25 Daniel 5.23 Job 33.4
6 Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa;Luc 2.32 Actes 13.47 Esaïe 49.8 Esaïe 49.6 Jérémie 23.5-23.6
7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.Esaïe 61.1 Esaïe 35.5 Esaïe 49.9 Hébreux 2.14-2.15 2 Timothée 2.26
8 Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.Esaïe 48.11 Exode 20.3-20.5 Psaumes 83.18 Esaïe 43.11 Exode 34.14
9 Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.Esaïe 43.19 Esaïe 46.9-46.10 1 Rois 8.15-8.20 2 Pierre 1.19-1.21 Esaïe 41.22-41.23
10 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo.Psaumes 33.3 Psaumes 40.3 Esaïe 42.4 Romains 15.9-15.11 Esaïe 24.14-24.16
11 Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele vya milima.Esaïe 32.16 Esaïe 60.7 Nahum 1.15 Genèse 25.23 Psaumes 72.8-72.10
12 Na wamtukuze Bwana, Na kutangaza sifa zake visiwani.Psaumes 117.1-117.2 Psaumes 22.27 Apocalypse 7.9-7.12 Esaïe 66.18-66.19 Apocalypse 5.9-5.10
13 Bwana atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu.Nahum 1.2 Psaumes 78.65 Osée 11.10 Jérémie 25.30 Esaïe 59.16-59.19
14 Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja.Psaumes 50.2 Job 32.18 Ecclésiaste 8.11-8.12 2 Pierre 3.9-3.10 2 Pierre 3.15
15 Nitaharibu milima na vilima, nitavikausha vyote vimeavyo; nitaifanya mito ya maji kuwa visiwa, na kuyakausha maziwa ya maji.Esaïe 50.2 Nahum 1.4-1.6 Esaïe 44.27 Esaïe 2.12-2.16 Esaïe 11.15-11.16
16 Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha.Esaïe 30.21 Ephésiens 5.8 Esaïe 32.3 Luc 3.5 Esaïe 40.4
17 Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu.Psaumes 97.7 Esaïe 1.29 Esaïe 44.11 Habakuk 2.18-2.20 Esaïe 44.17
18 Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona.Esaïe 29.18 Marc 7.34-7.37 Esaïe 43.8 Proverbes 20.12 Luc 7.22
19 Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa Bwana?Jérémie 5.21 2 Corinthiens 4.4 Ezéchiel 12.2 2 Corinthiens 3.14-3.15 Matthieu 23.16-23.24
20 Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii.Esaïe 58.2 Ezéchiel 33.31 Jean 11.37-11.50 Deutéronome 29.2-29.4 Jérémie 42.2-42.5
21 Bwana akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.Jean 15.10 1 Jean 3.4-3.5 Psaumes 71.16 Psaumes 71.19 Jean 17.4-17.5
22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.Esaïe 14.17 Deutéronome 28.29-28.33 Esaïe 18.2 Esaïe 52.4-52.5 Esaïe 24.18
23 Ni nani miongoni mwenu atakayetega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao?Esaïe 48.18 Actes 3.19 Matthieu 21.28-21.31 1 Pierre 4.2-4.3 Jérémie 3.4-3.7
24 Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang’anyi? Si yeye, Bwana? Yeye tuliyemkosa, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.Juges 10.7 Matthieu 22.7 Lamentations 1.18 Esaïe 45.7 Néhémie 9.26-9.27
25 Kwa sababu hiyo alimwaga ukali wa hasira yake juu yake, na nguvu za vita; ukawasha moto wa kumzunguka pande zote, wala hakujua; ukamteketeza, wala hakuyatia hayo moyoni mwake.Osée 7.9 Esaïe 57.11 2 Rois 25.9 Esaïe 57.1 Deutéronome 32.22

Cette Bible est dans le domaine public.