Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 28.16
Bible en Swahili de l’est


1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.Deutéronome 28.7 Psaumes 53.5 Lévitique 26.17 1 Thessaloniciens 2.2 Actes 14.3
2 Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwaGenèse 45.5-45.8 Ecclésiaste 9.15 2 Chroniques 32.20-32.26 1 Rois 15.28 1 Rois 15.25
3 Mtu mhitaji awaoneaye maskini, Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula.Matthieu 18.28-18.30
4 Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao.Ephésiens 5.11 Matthieu 14.4 Matthieu 3.7 Romains 1.32 1 Rois 18.18
5 Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao Bwana huelewa na yote.Jean 7.17 1 Jean 2.27 1 Jean 2.20 Psaumes 92.6 Jacques 1.5
6 Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.Proverbes 19.1 Luc 16.19-16.23 Proverbes 19.22 Proverbes 28.18 Actes 24.24-24.27
7 Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima; Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye.Proverbes 2.1-2.6 Proverbes 29.3 1 Pierre 4.3-4.4 Proverbes 23.19-23.22 Proverbes 3.1-3.35
8 Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.Proverbes 13.22 Lévitique 25.36 Proverbes 14.31 Exode 22.25 Proverbes 19.7
9 Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo.Psaumes 109.7 Psaumes 66.18 Zacharie 7.11-7.13 Esaïe 1.15-1.16 Proverbes 15.8
10 Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.Matthieu 6.33 Proverbes 26.27 Psaumes 37.25-37.26 Proverbes 15.6 Deutéronome 7.12-7.14
11 Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe; Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana.Romains 12.16 Proverbes 26.16 Ecclésiaste 9.15-9.17 Proverbes 19.1 Ezéchiel 28.3-28.5
12 Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha.Proverbes 29.2 Proverbes 11.10 Proverbes 28.28 Ecclésiaste 10.16 2 Chroniques 30.22-30.27
13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.Job 31.33 Psaumes 32.3-32.5 1 Jean 1.8-1.10 Jérémie 2.22-2.23 Daniel 9.20-9.23
14 Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara.Proverbes 23.17 Esaïe 66.2 Jérémie 32.40 Job 9.4 Exode 14.23
15 Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini.Matthieu 2.16 1 Pierre 5.8 Exode 1.22 2 Rois 21.16 2 Rois 15.16
16 Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.Esaïe 3.12 Amos 4.1 Néhémie 5.15 Esaïe 33.15-33.16 Jérémie 22.15-22.17
17 Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.Genèse 9.6 Exode 21.14 1 Rois 21.19 Actes 28.4 2 Rois 9.26
18 Aendaye kwa unyofu ataokolewa; Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara.Proverbes 10.9 Proverbes 28.6 Proverbes 10.25 Nombres 22.32 Psaumes 84.11
19 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.Proverbes 12.11 Proverbes 27.23-27.27 Proverbes 13.20 Luc 15.12-15.17 Juges 9.4
20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.Proverbes 20.21 Proverbes 13.11 Luc 16.10-16.12 Proverbes 28.22 1 Corinthiens 4.2-4.5
21 Kupendelea watu si kwema; Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate.Ezéchiel 13.19 Proverbes 24.23 Proverbes 18.5 Michée 7.3 Michée 3.5
22 Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjilia.Proverbes 23.6 Proverbes 28.20 1 Timothée 6.9 Marc 7.22 Job 27.16-27.17
23 Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali; Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake.Proverbes 27.5-27.6 Matthieu 18.15 1 Rois 1.23 Psaumes 141.5 2 Pierre 3.15-3.16
24 Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.Proverbes 18.9 Proverbes 19.26 Matthieu 15.4-15.6 Juges 17.2 Proverbes 28.7
25 Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina; Bali amtumainiye Bwana atawandishwa.Proverbes 15.18 Proverbes 11.25 1 Timothée 6.6 Proverbes 13.4 Jérémie 17.7-17.8
26 Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.Proverbes 3.5 Job 28.28 Jacques 3.13-3.18 Marc 14.27-14.31 Jacques 1.5
27 Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.Proverbes 19.17 Deutéronome 15.7 Proverbes 22.9 Proverbes 11.26 Psaumes 41.1-41.3
28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.Proverbes 28.12 Proverbes 29.2 Actes 12.23-12.24 Job 24.4 Esther 8.17

Cette Bible est dans le domaine public.