Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 96.8
Bible en Swahili de l’est


1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote.Psaumes 33.3 1 Chroniques 16.23-16.33 Psaumes 98.1 Psaumes 67.3-67.6 Apocalypse 5.9
2 Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.Psaumes 71.15 Marc 16.15 Psaumes 145.1 Psaumes 103.20-104.1 Psaumes 145.10
3 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.Psaumes 72.18-72.19 Daniel 6.26-6.27 Michée 4.2 Esaïe 19.23-19.25 Esaïe 49.6
4 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.Psaumes 18.3 Psaumes 89.7 Psaumes 95.3 Psaumes 145.3 Exode 18.11
5 Maana miungu yote ya watu si kitu, Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.Psaumes 115.15 Esaïe 42.5 Jérémie 10.11-10.12 Jérémie 10.14-10.15 Actes 19.26
6 Heshima na adhama ziko mbele zake, Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.Psaumes 104.1 Psaumes 29.1-29.2 Psaumes 19.1 2 Pierre 1.16-1.17 Psaumes 63.2-63.3
7 Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu.Psaumes 22.27 Psaumes 29.1-29.2 Apocalypse 19.1 1 Chroniques 29.11-29.13 1 Pierre 5.11
8 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake, Leteni sadaka mkaziingie nyua zake.Psaumes 100.4 Psaumes 108.3-108.5 Hébreux 13.15-13.16 Psaumes 72.10 Psaumes 45.12
9 Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote.Psaumes 29.2 Psaumes 33.8 Psaumes 114.7 Psaumes 110.3 Ezéchiel 7.20
10 Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili.Psaumes 93.1 Psaumes 9.8 Psaumes 67.4 Esaïe 49.8 Romains 3.5-3.6
11 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, Bahari na ivume na vyote viijazavyo,Esaïe 49.13 Psaumes 69.34 Psaumes 98.7-98.9 Psaumes 97.1 Luc 15.10
12 Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo, Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha;Esaïe 55.12-55.13 Psaumes 65.12-65.13 Esaïe 42.10-42.11 Esaïe 44.23 Esaïe 35.1
13 Mbele za Bwana, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.Apocalypse 19.11 Psaumes 98.9 Psaumes 67.4 1 Thessaloniciens 4.16-4.18 Apocalypse 11.18

Cette Bible est dans le domaine public.