Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 36.11
Bible en Swahili de l’est


1 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.Romains 3.18 Psaumes 18.1 Apocalypse 1.1 2 Pierre 1.1 Jude 1.1
2 Kwa maana hujipendekeza machoni pake Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.Deutéronome 29.19 Psaumes 49.18 Psaumes 10.3 Romains 7.9 Osée 12.7-12.8
3 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.Psaumes 55.21 Jérémie 4.22 Psaumes 10.7 Psaumes 12.2-12.3 1 Jean 2.19
4 Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii.Esaïe 65.2 Michée 2.1 Proverbes 4.16 Romains 12.9 Psaumes 97.10
5 Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni.Psaumes 57.10 Psaumes 103.11 Psaumes 108.4 Psaumes 52.1 Esaïe 55.7-55.9
6 Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee Bwana, unawaokoa wanadamu na wanyama.Romains 11.33 Psaumes 71.19 Psaumes 77.19 Psaumes 145.9 Psaumes 92.5
7 Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.Ruth 2.12 Psaumes 91.4 Psaumes 17.8 Psaumes 139.17 Psaumes 31.19
8 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.Psaumes 65.4 Psaumes 16.11 Esaïe 25.6 Jérémie 31.12-31.14 Esaïe 58.11
9 Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru.Jérémie 2.13 1 Pierre 2.9 Jean 4.14 Jean 4.10 Proverbes 4.18
10 Uwadumishie wakujuao fadhili zako, Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.Jérémie 22.16 Psaumes 97.10-97.11 Psaumes 103.17 1 Pierre 1.5 Jean 17.3
11 Mguu wa kiburi usinikaribie, Wala mkono wa wasio haki usinifukuze.Psaumes 62.6 Esaïe 51.23 Psaumes 119.85 Psaumes 17.8-17.14 Psaumes 119.122
12 Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu; Wameangushwa chini wasiweze kusimama.Psaumes 1.5 Apocalypse 19.1-19.6 2 Thessaloniciens 1.8-1.9 Psaumes 140.10 Psaumes 18.38

Cette Bible est dans le domaine public.