Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Chroniques 13.9
Bible en Swahili de l’est


1 Katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu, akaanza Abiya kutawala juu ya Yuda.2 Chroniques 12.16 1 Rois 15.1-15.8
2 Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka binti Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.2 Chroniques 11.20 1 Rois 15.6-15.7 Josué 18.28 Juges 19.14 1 Samuel 10.26
3 Abiya akapanga vita mwenye jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule mia nne elfu; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake mwenye watu wateule mia nane elfu, waliokuwa waume mashujaa.2 Chroniques 26.12-26.13 2 Chroniques 14.8-14.9 2 Chroniques 11.1 2 Chroniques 17.14-17.18 1 Samuel 17.1-17.3
4 Basi Abiya akasimama juu ya kilima cha Semaraimu, kilichoko milimani mwa Efraimu, akasema, Nisikieni, enyi Yeroboamu na Israeli wote;Josué 18.22 2 Chroniques 15.2 Juges 9.7 Genèse 10.18
5 je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi?Nombres 18.19 Lévitique 2.13 2 Samuel 7.12-7.16 Marc 9.49-9.50 Psaumes 89.19-89.37
6 Lakini Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumwa wa Sulemani mwana wa Daudi, akainuka, akamfanyia fitina bwana wake.1 Rois 11.26 1 Rois 12.20 1 Rois 12.27 2 Chroniques 10.19
7 Wakamkusanyikia watu mabaradhuli, wasiofaa kitu, waliojitia nguvu juu ya Rehoboamu mwana wa Sulemani, Rehoboamu alipokuwa kijana na wa moyo mwororo, asiweze kuwazuia.Juges 9.4 2 Chroniques 12.13 Deutéronome 13.13 Job 30.8 Hébreux 5.12
8 Hata sasa mwajidhania kuwa mtauzuia ufalme wa Bwana mikononi mwa wana wa Daudi; nanyi mmekuwa jamii kubwa, na kwenu mna ndama za dhahabu alizowafanyia Yeroboamu kuwa miungu.1 Rois 12.28 2 Chroniques 11.15 Psaumes 2.1-2.6 2 Chroniques 9.8 Osée 8.5-8.6
9 Je! Hamkuwafukuza makuhani wa Bwana, wana wa Haruni, na Walawi; mkajifanyia makuhani kama wafanyavyo watu wa nchi nyingine? Hata ye yote ajaye kujifanya wakfu na ndama, na kondoo waume saba, aweza kuwa kuhani wa hiyo isiyo miungu.2 Chroniques 11.14-11.15 Jérémie 2.11 Exode 29.35 1 Chroniques 29.5 Actes 19.26
10 Lakini sisi, Bwana ndiye Mungu wetu, wala sisi hatukumwacha; tena tunao makuhani wanaomtumikia Bwana, wana wa Haruni, na Walawi, kwa kazi yao;2 Chroniques 11.16-11.17 Exode 19.5-19.6 Zacharie 13.9 Nombres 16.40 Exode 29.1-29.37
11 nao humtolea Bwana kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi twayalinda malinzi ya Bwana, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha.2 Chroniques 2.4 Lévitique 24.2-24.9 Exode 29.38 Exode 25.30-25.39 Exode 27.20-27.21
12 Na tazama, Mungu yu pamoja nasi atutangulie, na makuhani wake wenye mapanda, ili wapige sauti ya kugutusha juu yenu. Enyi wana wa Israeli, msipigane na Bwana, Mungu wa baba zenu; kwani hamtafanikiwa.Nombres 10.8-10.9 Actes 5.39 Zacharie 10.5 Josué 6.13-6.20 Psaumes 20.7
13 Lakini Yeroboamu aliwazungushia waviziao kwa nyuma; basi wao wakawa mbele ya Yuda, na wale waviziao nyuma yao.Josué 8.9 Josué 8.4 Jérémie 4.22 2 Chroniques 20.22 Proverbes 21.30
14 Na Yuda walipotazama nyuma, angalia, vita vikawa mbele na nyuma; wakamlilia Bwana, na makuhani wakapiga mapanda.2 Chroniques 14.11 Juges 20.33-20.43 2 Samuel 10.8-10.14 Exode 14.10 Josué 8.20
15 Ndipo wakapiga kelele watu wa Yuda; ikawa, watu na Yuda walipopiga kelele, Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.2 Chroniques 14.12 Psaumes 118.4-118.7 Juges 4.15 2 Chroniques 20.21 Nombres 32.4
16 Wana wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda; naye Mungu akawaua mikononi mwao.2 Chroniques 16.8 1 Samuel 23.7 Deutéronome 3.3 Josué 21.44 Genèse 14.20
17 Abiya na watu wake wakawapiga mapigo makuu; hata wakaanguka wameuawa wa Israeli mia tano elfu, watu wateule.Esaïe 37.36 2 Chroniques 13.12 2 Chroniques 13.3 1 Corinthiens 10.22 Nahum 1.5
18 Ndivyo walivyotiishwa wana wa Israeli wakati ule, wakashinda wana wa Yuda, kwa kuwa walimtegemea Bwana, Mungu wa baba zao.2 Chroniques 14.11 1 Chroniques 5.20 Daniel 3.28 2 Chroniques 16.8-16.9 2 Chroniques 20.20
19 Abiya akamfuata Yeroboamu, akamnyang’anya miji, Betheli na miji yake, na Yeshana na miji yake, na Efroni na miji yake.2 Chroniques 15.8 Josué 15.9 Josué 11.12 Josué 10.19 Jean 11.54
20 Wala Yeroboamu hakupata nguvu tena siku za Abiya; kisha Bwana akampiga, akafa.1 Samuel 25.38 1 Rois 14.20 Actes 12.23 Psaumes 18.37-18.38 1 Samuel 26.10
21 Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana ishirini na wawili, na binti kumi na sita.2 Chroniques 11.21 Juges 10.4 Juges 9.5 2 Samuel 5.12-5.13 Juges 8.30-8.31
22 Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.2 Chroniques 9.29 2 Chroniques 12.15 2 Chroniques 24.27

Cette Bible est dans le domaine public.