1  Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 
Jean 20.27  Actes 4.20  1 Jean 4.14  Luc 24.39  Jean 5.26  
 2  (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 
1 Jean 3.8  1 Jean 5.20  Jean 1.4  1 Jean 3.5  Jean 17.3  
 3  hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 
1 Jean 1.1  1 Corinthiens 1.9  Philippiens 2.1  Jean 17.21  Jean 17.3  
 4  Na haya twayaandika, ili furaha yetu itimizwe. 
Jean 15.11  Jean 16.24  1 Jean 2.1  Jean 3.29  2 Jean 1.12  
 5  Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake. 
Jean 8.12  Jacques 1.17  Psaumes 27.1  Esaïe 60.19  1 Timothée 6.16  
 6  Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; 
1 Jean 4.20  1 Jean 1.10  Jean 3.19-3.21  1 Jean 2.4  Jean 8.12  
 7  bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 
Ephésiens 1.7  Ephésiens 5.8  Apocalypse 1.5  Romains 13.12  1 Timothée 6.16  
 8  Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. 
1 Jean 2.4  Jacques 3.2  Job 15.14  Romains 3.23  Esaïe 53.6  
 9  Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. 
Psaumes 32.5  Proverbes 28.13  1 Jean 1.7  Psaumes 51.2-51.5  Jérémie 33.8  
 10  Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu. 
1 Jean 5.10  1 Jean 1.8  Psaumes 130.3  1 Jean 2.14  Job 24.25