1  Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana. 
Galates 2.2  Galates 1.12  2 Corinthiens 12.7  Joël 2.28-2.29  Daniel 10.5-10.10  
 2  Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. 
2 Corinthiens 11.11  1 Thessaloniciens 4.17  Apocalypse 12.5  Actes 22.17  Romains 16.7  
 3  Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);  
4  ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene. 
Luc 23.43  Apocalypse 2.7  Ezéchiel 31.9  
 5  Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu. 
1 Corinthiens 2.3  2 Corinthiens 12.9-12.10  2 Corinthiens 11.30  
 6  Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu. 
2 Corinthiens 11.16  2 Corinthiens 11.31  2 Corinthiens 12.7  2 Corinthiens 12.11  Job 24.25  
 7  Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. 
1 Corinthiens 5.5  Daniel 5.20  Juges 2.3  2 Chroniques 26.16  Nombres 33.55  
 8  Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. 
2 Samuel 12.16-12.18  Hébreux 5.7  1 Samuel 15.11  Psaumes 77.2-77.11  Matthieu 20.21-20.22  
 9  Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 
2 Corinthiens 12.10  Philippiens 4.13  Ephésiens 3.16  Esaïe 40.29-40.31  1 Corinthiens 10.13  
 10  Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. 
2 Corinthiens 13.4  Romains 5.3  2 Corinthiens 6.4  2 Corinthiens 12.9  Jacques 1.2  
 11  Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lo lote, nijapokuwa si kitu. 
2 Corinthiens 11.5  2 Corinthiens 11.1  2 Corinthiens 1.6  Ephésiens 3.8  2 Corinthiens 12.12  
 12  Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza. 
Romains 15.18-15.19  2 Corinthiens 6.4-6.10  1 Corinthiens 1.5-1.7  1 Corinthiens 14.18  2 Corinthiens 11.4  
 13  Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila kwa kuwa mimi sikuwalemea? Mnisamehe udhalimu huu. 
1 Corinthiens 9.12  2 Corinthiens 12.14  1 Corinthiens 9.6  2 Corinthiens 11.7-11.9  1 Corinthiens 9.15-9.18  
 14  Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto. 
Proverbes 19.14  2 Corinthiens 1.15  1 Corinthiens 4.14-4.15  1 Corinthiens 10.33  Proverbes 13.22  
 15  Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa? 
1 Thessaloniciens 2.8  Philippiens 2.17  2 Corinthiens 1.6  Colossiens 1.24  2 Corinthiens 2.3  
 16  Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila. 
1 Thessaloniciens 2.5  1 Thessaloniciens 2.3  2 Corinthiens 1.12  2 Corinthiens 7.2  2 Corinthiens 12.13  
 17  Je! Mtu ye yote niliyemtuma kwenu, kwa mtu huyo naliwatoza kitu? 
1 Corinthiens 16.10  1 Corinthiens 4.17  2 Rois 5.16  2 Corinthiens 12.18  2 Corinthiens 9.5  
 18  Nalimwonya Tito, nikamtuma ndugu yule pamoja naye. Je! Tito aliwatoza kitu? Je! Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile? 
2 Corinthiens 8.6  Romains 4.12  Philippiens 2.19-2.22  2 Corinthiens 7.2  Nombres 16.15  
 19  Mwadhani hata sasa ya kuwa najidhuru kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi. 
Romains 9.1  2 Corinthiens 10.8  1 Corinthiens 14.26  1 Corinthiens 10.33  Philippiens 4.1  
 20  Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong’onezo, na majivuno, na ghasia; 
1 Corinthiens 1.11  Romains 1.29  1 Pierre 2.1  Galates 5.15  1 Corinthiens 14.33  
 21  nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya. 
2 Corinthiens 13.2  Colossiens 3.5  Galates 5.19  1 Corinthiens 5.1  1 Corinthiens 5.9-5.11