Jonas dans le poisson
 1  Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, 
Psaumes 130.1-130.2  Job 13.15  Osée 5.15-6.3  Lamentations 3.53-3.56  2 Chroniques 33.11-33.13  
 2  Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. 
Psaumes 18.4-18.6  Psaumes 120.1  Psaumes 34.6  Psaumes 65.2  Matthieu 12.40  
 3  Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. 
Psaumes 42.7  Lamentations 3.54  Psaumes 69.14-69.15  Psaumes 69.1-69.2  Psaumes 88.5-88.8  
 4  Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu. 
Psaumes 31.22  Psaumes 5.7  2 Chroniques 6.38  Jérémie 7.15  Daniel 6.10  
 5  Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu; 
Psaumes 69.1-69.2  Lamentations 3.54  Psaumes 40.2  
 6  Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, 
Psaumes 30.3  Psaumes 16.10  Esaïe 38.17  Psaumes 55.23  Psaumes 143.7  
 7  Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. 
Psaumes 11.4  Psaumes 18.6  2 Chroniques 30.27  Jonas 2.4  Michée 1.2  
 8  Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; 
Psaumes 31.6  Jérémie 2.13  2 Rois 17.15  1 Samuel 12.21  Jérémie 10.8  
 9  Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana. 
Psaumes 3.8  Psaumes 50.14  Osée 14.2  Ecclésiaste 5.4-5.5  Esaïe 45.17  
 10  Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani. 
Matthieu 8.8-8.9  Jonas 1.17  Genèse 1.7  Psaumes 105.31  Genèse 1.3