1 Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.
Osée 6.1  Osée 12.6  Osée 13.9  2 Chroniques 30.6-30.9  Lamentations 5.16  
Appel à revenir à Dieu et promesses
 2 Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe.
Hébreux 13.15  Luc 18.13  Psaumes 69.30-69.31  Luc 11.13  Hébreux 10.4  
 3 Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.Psaumes 10.14  Psaumes 68.5  Psaumes 33.17  Osée 14.8  Osée 5.13  
 4 Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha.
Esaïe 57.18  Sophonie 3.17  Esaïe 12.1  Ephésiens 2.4-2.9  Osée 6.1  
 5 Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni.
Esaïe 35.2  Matthieu 6.28  Esaïe 27.6  Esaïe 26.19  Proverbes 19.12  
 6 Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.
Psaumes 52.8  Jérémie 11.16  Genèse 27.27  Psaumes 80.9-80.11  Psaumes 128.3  
 7 Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni.
Psaumes 91.1  Esaïe 61.11  Zacharie 8.12  Osée 14.5  Psaumes 85.6  
 8 Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.
Esaïe 41.19  Job 34.32  1 Pierre 1.14-1.16  Jean 1.16  Jean 15.1-15.8  
 9 Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Psaumes 107.43  Proverbes 10.29  Sophonie 3.5  Jérémie 9.12  Deutéronome 32.4