Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 14.3
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.Osée 6.1 Osée 12.6 Osée 13.9 2 Chroniques 30.6-30.9 Joël 2.12-2.13
2 Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe.Hébreux 13.15 Luc 18.13 Psaumes 69.30-69.31 Hébreux 10.4 Zacharie 3.4
3 Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.Psaumes 10.14 Psaumes 68.5 Psaumes 33.17 Osée 5.13 Esaïe 30.16
4 Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha.Esaïe 57.18 Sophonie 3.17 Esaïe 12.1 Ephésiens 2.4-2.9 Osée 6.1
5 Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni.Esaïe 35.2 Matthieu 6.28 Esaïe 27.6 Esaïe 26.19 Proverbes 19.12
6 Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.Psaumes 52.8 Genèse 27.27 Psaumes 80.9-80.11 Psaumes 128.3 Cantique 4.11-4.15
7 Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni.Psaumes 91.1 Zacharie 8.12 Osée 14.5 Psaumes 85.6 Ezéchiel 17.23
8 Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.Esaïe 41.19 Job 34.32 Jean 15.1-15.8 Actes 19.18-19.20 Philippiens 1.11
9 Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.Psaumes 107.43 Proverbes 10.29 Sophonie 3.5 Jérémie 9.12 Jean 8.47

Cette Bible est dans le domaine public.