Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 14.2
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.Osée 6.1 Osée 12.6 Osée 13.9 2 Chroniques 30.6-30.9 Osée 5.5
2 Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe.Hébreux 13.15 Psaumes 69.30-69.31 Luc 18.13 1 Pierre 2.9 1 Jean 3.5
3 Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.Psaumes 68.5 Psaumes 10.14 Psaumes 33.17 Esaïe 31.1 Osée 14.8
4 Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha.Jérémie 3.22 Esaïe 57.18 Sophonie 3.17 Esaïe 12.1 Ephésiens 2.4-2.9
5 Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni.Esaïe 35.2 Matthieu 6.28 Deutéronome 32.2 Job 29.19 Esaïe 27.6
6 Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.Psaumes 52.8 Philippiens 4.18 Jean 15.1 2 Corinthiens 2.14-2.15 Ezéchiel 31.3-31.10
7 Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni.Psaumes 91.1 Jean 12.24 Osée 2.22 Psaumes 138.7 Osée 6.2
8 Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.Job 34.32 Esaïe 41.19 Osée 14.2-14.3 Esaïe 60.13 1 Thessaloniciens 1.9
9 Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.Psaumes 107.43 Proverbes 10.29 Jérémie 9.12 Sophonie 3.5 Daniel 12.10

Cette Bible est dans le domaine public.