Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 52.3
Bible en Swahili de l’est


1 Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.Apocalypse 21.27 Esaïe 51.17 Esaïe 48.2 Esaïe 35.8 Néhémie 11.1
2 Jikung’ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa.Jérémie 51.45 Zacharie 2.6 Luc 21.24 Jérémie 51.50 Esaïe 29.4
3 Maana Bwana asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.Esaïe 45.13 Psaumes 44.12 1 Pierre 1.18 Jérémie 15.13 Esaïe 50.1
4 Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu.Genèse 46.6 Jean 15.25 Jérémie 50.17 Job 2.3 Psaumes 25.3
5 Basi sasa, nafanya nini hapa, asema Bwana, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema Bwana, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.Romains 2.24 Esaïe 52.3 Exode 2.23-2.24 Psaumes 74.10 Esaïe 51.20
6 Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.Ezéchiel 37.13-37.14 Hébreux 8.10-8.11 Ezéchiel 39.27-39.29 Exode 33.19 Esaïe 49.23
7 Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!Romains 10.12-10.15 Esaïe 40.9 Nahum 1.15 Luc 2.10 Psaumes 93.1
8 Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni.Esaïe 62.6 1 Corinthiens 13.12 Actes 2.46-2.47 Actes 4.32 Esaïe 48.20
9 Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa Bwana amewafariji watu wake, Ameukomboa Yerusalemu.Esaïe 51.3 Psaumes 98.4 Psaumes 96.11-96.12 Esaïe 44.23 Esaïe 44.26
10 Bwana ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.Esaïe 51.9 Psaumes 98.1-98.3 Luc 3.6 Esaïe 49.6 Apocalypse 11.15-11.17
11 Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.2 Corinthiens 6.17 Esaïe 48.20 Zacharie 2.6-2.7 Jérémie 50.8 Apocalypse 18.4
12 Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu Bwana atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.Esaïe 58.8 Michée 2.13 Esaïe 45.2 Exode 12.39 Exode 13.21-13.22
13 Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.Matthieu 28.18 Esaïe 42.1 Philippiens 2.7-2.11 Hébreux 1.3 Esaïe 53.10-53.11
14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),Esaïe 53.2-53.5 Matthieu 26.67 Psaumes 22.17 Matthieu 22.22-22.23 Marc 7.37
15 ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.Esaïe 49.7 Ezéchiel 36.25 Romains 15.20-15.21 Esaïe 49.23 Matthieu 28.19

Cette Bible est dans le domaine public.