Bénédiction future d’Israël
 1  Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. 
Esaïe 51.3  Esaïe 55.12-55.13  Esaïe 27.6  Ezéchiel 36.35  Esaïe 41.18-41.19  
 2  Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu. 
Esaïe 60.13  Esaïe 25.9  Esaïe 40.5  Esaïe 55.12-55.13  Esaïe 60.1-60.3  
 3  Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea. 
Hébreux 12.12  Job 4.3-4.4  Actes 18.23  Job 16.5  Juges 7.11  
 4  Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. 
Esaïe 34.8  Apocalypse 1.7  Esaïe 61.2  Esaïe 28.16  Esaïe 32.4  
 5  Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. 
Esaïe 32.3-32.4  Esaïe 42.6-42.7  Esaïe 29.18  Esaïe 50.4  Ephésiens 5.14  
 6  Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. 
Jean 5.8-5.9  Luc 11.14  Matthieu 12.22  Matthieu 9.32-9.33  Esaïe 32.4  
 7  Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi. 
Esaïe 34.13  Esaïe 13.22  Esaïe 49.10  Matthieu 21.43  Esaïe 19.6  
 8  Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. 
Matthieu 7.13-7.14  Tite 2.11-2.14  Hébreux 12.14  Ezéchiel 44.9  Esaïe 11.16  
 9  Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. 
Esaïe 62.12  Esaïe 30.6  Ezéchiel 34.25  Galates 3.13  Apocalypse 20.1-20.3  
 10  Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia. 
Apocalypse 21.4  Esaïe 25.8  Esaïe 65.19  Esaïe 30.19  Psaumes 84.7