Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 35
Bible en Swahili de l’est


1 Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Esaïe 51.3 Esaïe 55.12-55.13 Esaïe 27.10 Psaumes 48.11 Esaïe 40.3
2 Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu. Esaïe 60.13 Esaïe 25.9 Esaïe 60.1-60.3 Romains 10.15 Esaïe 40.5
3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea. Hébreux 12.12 Job 4.3-4.4 Esaïe 52.1-52.2 Luc 22.32 Luc 22.43
4 Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. Esaïe 34.8 Malachie 3.1 Apocalypse 1.7 Esaïe 61.2 Esaïe 28.16
5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. Esaïe 29.18 Esaïe 32.3-32.4 Esaïe 42.6-42.7 Esaïe 50.4 Jean 9.39
6 Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. Jean 5.8-5.9 Luc 11.14 Matthieu 12.22 Matthieu 9.32-9.33 Esaïe 32.4
7 Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi. Esaïe 49.10 Esaïe 34.13 Esaïe 13.22 1 Corinthiens 6.9-6.11 Esaïe 29.17
8 Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. Matthieu 7.13-7.14 Tite 2.11-2.14 Hébreux 12.14 Esaïe 62.10 Esaïe 40.3-40.4
9 Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. Esaïe 62.12 Apocalypse 5.9 Esaïe 63.4 Tite 2.14 Exode 15.13
10 Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia. Apocalypse 21.4 Esaïe 30.19 Esaïe 25.8 Esaïe 65.19 Jérémie 31.11-31.14

Cette Bible est dans le domaine public.