Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 31
Bible en Swahili de l’est


1 Ole wao watelemkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Bwana! Psaumes 20.7 Deutéronome 17.16 Daniel 9.13 Esaïe 30.16 Esaïe 36.6
2 Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu. Nombres 23.19 Esaïe 45.7 Psaumes 78.65-78.66 Esaïe 28.21 Josué 23.15
3 Basi Wamisri ni wanadamu wala si Mungu, na farasi zao ni nyama wala si roho; na Bwana atakaponyosha mkono wake, yeye asaidiaye atajikwaa, na yeye asaidiwaye ataanguka, nao wote pamoja watakoma. Esaïe 9.17 Ezéchiel 28.9 Ezéchiel 20.33-20.34 Jérémie 15.6 Esaïe 30.7
4 Maana Bwana aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwana-simba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo Bwana wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake. Amos 3.8 Esaïe 42.13 Osée 11.10 Zacharie 12.8 Psaumes 125.1-125.2
5 Kama ndege warukao, Bwana wa majeshi ataulinda Yerusalemu; ataulinda na kuuokoa, atapita juu yake na kuuhifadhi. Deutéronome 32.11 Psaumes 91.4 Esaïe 38.6 Esaïe 37.35 Psaumes 46.5
6 Mwelekeeni yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli. Jérémie 3.14 Esaïe 55.7 Jérémie 3.10 Jérémie 3.22 Jérémie 5.23
7 Maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu. Esaïe 30.22 Esaïe 2.20 1 Rois 12.28-12.30 Deutéronome 7.25 Ezéchiel 36.25
8 Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi. Esaïe 14.25 Genèse 49.15 Esaïe 37.35-37.38 Esaïe 29.5 Esaïe 10.16-10.19
9 Na mwamba wake utatoweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema Bwana, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuru yake katika Yerusalemu. Esaïe 29.6 Esaïe 18.3 Zacharie 2.5 Esaïe 4.4 Lévitique 6.13

Cette Bible est dans le domaine public.