Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ecclésiaste 3.3
Bible en Swahili de l’est


1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.Ecclésiaste 3.17 Ecclésiaste 8.5-8.6 2 Rois 5.26 Ecclésiaste 2.3 Matthieu 16.3
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;Hébreux 9.27 Job 14.5 Galates 4.4 Actes 7.20 Esaïe 5.2-5.5
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;Osée 6.1-6.2 1 Samuel 2.6 Jérémie 33.6 Esaïe 38.5-38.20 Ezéchiel 13.14
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;Exode 15.20 Romains 12.15 Jean 16.20-16.22 Jacques 4.9 2 Corinthiens 7.10
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;2 Rois 3.25 Joël 2.16 2 Samuel 18.17-18.18 Exode 19.15 Josué 4.3-4.9
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;Philippiens 3.7-3.8 Luc 9.24-9.25 Matthieu 16.25-16.26 Marc 8.35-8.37 2 Rois 7.15
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;Amos 5.13 Genèse 37.29 Genèse 44.18 Luc 19.37-19.40 Job 32.4-32.22
8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.Luc 14.26 Ephésiens 5.25 2 Chroniques 20.1-20.30 Ephésiens 5.28-5.29 Psaumes 139.21
9 Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?Ecclésiaste 1.3 Matthieu 16.26 Ecclésiaste 5.16 Proverbes 14.23 Ecclésiaste 2.11
10 Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.Genèse 3.19 Ecclésiaste 2.26 Ecclésiaste 1.13-1.14 1 Thessaloniciens 2.9 2 Thessaloniciens 3.8
11 Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.Romains 11.33 Romains 1.19-1.20 Ecclésiaste 8.17 Job 11.7 Genèse 1.31
12 Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi.Ecclésiaste 3.22 Psaumes 37.3 Philippiens 4.4-4.9 Ecclésiaste 9.7-9.9 Actes 20.35
13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.Ecclésiaste 2.24 Ecclésiaste 5.18-5.20 Psaumes 128.2 Esaïe 65.21-65.23 Ecclésiaste 9.7
14 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.Jacques 1.17 Psaumes 33.11 Romains 11.36 Proverbes 21.30 Psaumes 76.10
15 Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.Ecclésiaste 1.9-1.10 Ecclésiaste 6.10
16 Zaidi ya hayo, nikaona tena chini ya jua ya kwamba, Mahali pa hukumu upo uovu, Na mahali pa haki upo udhalimu.Ecclésiaste 4.1 Ecclésiaste 5.8 Michée 2.2 Actes 23.3 Psaumes 94.21-94.22
17 Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi.Matthieu 16.27 Ecclésiaste 3.1 2 Corinthiens 5.10 Psaumes 98.9 2 Thessaloniciens 1.6-1.10
18 Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.Psaumes 73.22 Genèse 3.17-3.19 Romains 9.23 1 Pierre 1.24 Psaumes 49.12
19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.Psaumes 49.12 Psaumes 49.20 2 Samuel 14.14 Psaumes 92.6-92.7 Ecclésiaste 2.16
20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.Genèse 3.19 Job 34.15 Job 10.9-10.10 Ecclésiaste 6.6 Ecclésiaste 12.7
21 Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?Ecclésiaste 12.7 Luc 16.22-16.23 Philippiens 1.23 2 Corinthiens 5.8 Actes 1.25
22 Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye.Ecclésiaste 6.12 Ecclésiaste 10.14 Ecclésiaste 2.24 Ecclésiaste 8.7 Ecclésiaste 3.11-3.12

Cette Bible est dans le domaine public.