Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 13.9
Bible en Swahili de l’est


1 Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye; Bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.Proverbes 15.20 Proverbes 10.1 Proverbes 9.7-9.8 Esaïe 28.14-28.15 Proverbes 4.20-4.22
2 Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri.Proverbes 12.14 Proverbes 18.20 Proverbes 1.31 Proverbes 1.11-1.13 Psaumes 140.11
3 Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.Proverbes 21.23 Proverbes 18.7 Jacques 3.2-3.12 Proverbes 18.21 Proverbes 12.13
4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.Proverbes 12.24 Proverbes 10.4 Proverbes 12.11 Proverbes 2.2-2.9 Proverbes 11.25
5 Mwenye haki huchukia kusema uongo; Bali mtu mbaya huwa karaha, hupatwa na aibu.Colossiens 3.9 Proverbes 3.35 Ezéchiel 6.9 Zacharie 11.8 Ezéchiel 20.43
6 Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake; Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi.Proverbes 11.3 Proverbes 11.5-11.6 Psaumes 140.11 2 Chroniques 28.23 Psaumes 26.1
7 Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu; Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.1 Corinthiens 4.10-4.11 Luc 18.11-18.14 Apocalypse 3.17 2 Corinthiens 6.10 Jacques 2.5
8 Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote.Exode 21.30 Jérémie 39.10 1 Pierre 1.18-1.19 Matthieu 16.26 Jérémie 41.8
9 Nuru ya mwenye haki yang’aa sana; Bali taa ya mtu mbaya itazimika.Proverbes 4.18 Proverbes 24.20 Matthieu 25.8 1 Rois 11.36 Job 29.3
10 Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.Jacques 4.1 3 Jean 1.9-1.10 1 Rois 12.10-12.11 Juges 12.1-12.6 Luc 14.28-14.32
11 Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.Proverbes 20.21 Proverbes 10.2 Jacques 5.1-5.5 Proverbes 28.8 Job 20.15
12 Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.Proverbes 13.19 Jean 16.22 Proverbes 11.30 1 Samuel 1.26-1.28 Psaumes 17.15
13 Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu; Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu.2 Chroniques 36.16 Nombres 15.31 Psaumes 115.13 2 Jean 1.8 Psaumes 19.11
14 Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.Proverbes 10.11 Proverbes 14.27 Psaumes 18.5 Proverbes 16.17 2 Samuel 22.6-22.7
15 Ufahamu mwema huleta upendeleo; Bali njia ya haini huparuza.Proverbes 3.4 Luc 2.52 Jérémie 2.19 Romains 6.21 Proverbes 15.10
16 Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu.Proverbes 15.2 Ecclésiaste 10.3 Proverbes 12.22-12.23 Esaïe 52.13 1 Samuel 25.25
17 Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya.Proverbes 25.13 Proverbes 25.23 1 Corinthiens 4.2 2 Timothée 2.2 Jérémie 23.28
18 Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa.Proverbes 15.5 Proverbes 15.31-15.32 Proverbes 12.1 Proverbes 25.12 Hébreux 12.25
19 Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.Proverbes 13.12 Proverbes 3.7 Psaumes 34.14 Proverbes 29.27 Cantique 3.4
20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.1 Corinthiens 15.33-15.34 Proverbes 9.6 2 Corinthiens 6.14-6.18 Proverbes 15.31 Apocalypse 18.4
21 Uovu huwaandamia wenye dhambi; Bali mwenye haki atalipwa mema.Psaumes 32.10 Proverbes 13.13 Romains 2.7-2.10 Esaïe 3.10-3.11 Genèse 4.7
22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.Proverbes 28.8 Job 27.16-27.17 Ecclésiaste 2.26 Genèse 17.7-17.8 Esdras 9.12
23 Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.Proverbes 12.11 Proverbes 28.19 Ecclésiaste 8.5-8.6 Jérémie 8.7-8.10 Ecclésiaste 5.9
24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.Proverbes 29.15 Proverbes 19.18 Proverbes 22.15 Proverbes 23.13-23.14 Proverbes 29.17
25 Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake; Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa.Psaumes 34.10 Proverbes 10.3 Hébreux 13.5 Deutéronome 32.24 Proverbes 6.11

Cette Bible est dans le domaine public.