Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 92
Bible en Swahili de l’est


1 Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. Psaumes 147.1 Ephésiens 5.19 Psaumes 135.3 Psaumes 107.21-107.22 Esaïe 57.15
2 Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku. Jean 1.17 Lamentations 3.22-3.23 Psaumes 42.8 Psaumes 89.1-89.2 Job 35.10
3 Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi. Psaumes 33.2 Néhémie 12.27 1 Chroniques 13.8 1 Samuel 10.5 Psaumes 81.2-81.3
4 Kwa kuwa umenifurahisha, Bwana, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako. 2 Corinthiens 2.14 Esaïe 65.13-65.14 Psaumes 8.6 Luc 1.47 Psaumes 106.47-106.48
5 Ee Bwana, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa. Esaïe 55.8-55.9 Psaumes 40.5 Romains 11.33-11.34 Psaumes 139.17 Psaumes 145.3-145.4
6 Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu. Psaumes 73.22 Psaumes 94.8 Psaumes 49.10 1 Corinthiens 2.14 Proverbes 1.22
7 Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele; Psaumes 37.38 Psaumes 73.18-73.20 1 Pierre 1.24 Job 12.6 Psaumes 37.35-37.36
8 Bali Wewe, Bwana, U Mtukufu hata milele. Psaumes 83.18 Actes 12.22-12.24 Actes 12.1 Psaumes 102.26-102.27 Psaumes 56.2
9 Maana hao adui zako, Ee Bwana, Hao adui zako watapotea, Na watendao maovu watatawanyika wote pia. Psaumes 37.20 Psaumes 89.10 Psaumes 1.4 Luc 19.27 Esaïe 17.13
10 Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi. Psaumes 23.5 Psaumes 45.7 Psaumes 89.17 Nombres 23.22 1 Samuel 2.10
11 Na jicho langu limewatazama walioniotea, Sikio langu limesikia habari za waovu walionishambulia. Psaumes 54.7 Psaumes 91.8 Psaumes 37.34 Psaumes 59.10 Psaumes 112.8
12 Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Psaumes 1.3 Psaumes 52.8 Esaïe 55.13 Jérémie 17.8 Nombres 24.6
13 Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu. Psaumes 100.4 Psaumes 135.2 Esaïe 60.21 Ephésiens 3.17 Romains 6.5
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Esaïe 46.4 Ezéchiel 47.12 Philippiens 1.11 Job 17.9 Psaumes 1.3
15 Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu. Psaumes 18.2 Romains 9.14 Psaumes 62.6 Job 34.10 Deutéronome 32.4

Cette Bible est dans le domaine public.