Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 77.6
Bible en Swahili de l’est


1 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.Psaumes 3.4 Psaumes 50.1 Psaumes 39.1 Psaumes 34.6 1 Chroniques 25.3
2 Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.Esaïe 26.9 Genèse 37.35 Psaumes 50.15 Esaïe 26.16 2 Rois 19.3-19.4
3 Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.Psaumes 61.2 Job 7.11 Job 6.4 Lamentations 3.39 Job 23.15-23.16
4 Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Naliona mashaka nisiweze kunena.Job 7.13-7.15 Job 6.3 Job 2.13 Esther 6.1 Psaumes 6.6
5 Nalifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita.Deutéronome 32.7 Psaumes 143.5 Esaïe 51.9 Psaumes 44.1 Michée 7.14-7.15
6 Nakumbuka wimbo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu ikatafuta.Psaumes 4.4 Psaumes 42.8 Jonas 1.2 Actes 16.25 1 Corinthiens 11.28-11.32
7 Je! Bwana atatupa milele na milele? Hatatenda fadhili tena kabisa?Psaumes 85.1 Psaumes 85.5 Psaumes 13.1-13.2 Psaumes 37.24 Psaumes 89.38
8 Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote?Nombres 23.19 Romains 9.6 Luc 16.25-16.26 Esaïe 27.11 Nombres 14.34
9 Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?Esaïe 49.14-49.15 Psaumes 25.6 Psaumes 40.11 Luc 13.25-13.28 Esaïe 40.27
10 Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu.Psaumes 31.22 Deutéronome 4.34 Exode 15.6 Habakuk 3.2-3.13 Job 42.3
11 Nitayakumbuka matendo ya Bwana; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.Psaumes 143.5 Psaumes 105.5 Psaumes 77.10 Psaumes 111.4 Esaïe 5.12
12 Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.Psaumes 104.34 Psaumes 71.24 Psaumes 145.11 Psaumes 145.4 Psaumes 143.5
13 Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?Exode 15.11 Psaumes 73.17 Deutéronome 32.31 Psaumes 63.2 Psaumes 89.6-89.8
14 Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.Daniel 6.27 Psaumes 136.4 Exode 13.14 Josué 9.9-9.10 Esaïe 51.9
15 Kwa mkono wako umewakomboa watu wako, Wana wa Yakobo na Yusufu.Exode 6.6 Deutéronome 9.29 Deutéronome 9.26 Psaumes 136.11-136.12 Psaumes 74.2
16 Ee Mungu, yale maji yalikuona, Yale maji yalikuona, yakaogopa. Vilindi vya maji navyo vikatetemeka,Exode 14.21 Josué 3.15-3.16 Habakuk 3.15 Psaumes 114.3-114.6 Habakuk 3.8-3.10
17 Mawingu yakamwaga maji. Mbingu nazo zikatoa sauti, Mishale yako nayo ikatapakaa.Psaumes 18.14 2 Samuel 22.15 Psaumes 144.6 Juges 5.4 Habakuk 3.11
18 Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli; Umeme uliuangaza ulimwengu. Nchi ilitetemeka na kutikisika;Psaumes 97.4 Matthieu 27.51 2 Samuel 22.8 Juges 5.4 Apocalypse 18.1
19 Njia yako ilikuwa katika bahari. Na mapito yako yalikuwa katika maji makuu; Hatua zako hazikujulikana.Habakuk 3.15 Nahum 1.3-1.4 Exode 14.28 Néhémie 9.11 Psaumes 29.10
20 Uliwaongoza watu wako kama kundi, Kwa mkono wa Musa na Haruni.Exode 13.21 Psaumes 78.52 Exode 14.19 Esaïe 63.11-63.12 Psaumes 80.1

Cette Bible est dans le domaine public.