Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 77.20
Bible en Swahili de l’est


1 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.Psaumes 3.4 Psaumes 39.1 Psaumes 50.1 1 Chroniques 16.41-16.42 Psaumes 142.1-142.3
2 Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.Psaumes 50.15 Esaïe 26.9 Genèse 37.35 Esaïe 26.16 Jonas 2.1-2.2
3 Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.Psaumes 61.2 Job 23.15-23.16 Job 31.23 Psaumes 88.3-88.18 Psaumes 42.11
4 Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Naliona mashaka nisiweze kunena.Job 2.13 Esther 6.1 Psaumes 6.6 Job 7.13-7.15 Job 6.3
5 Nalifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita.Deutéronome 32.7 Psaumes 143.5 Esaïe 51.9 Psaumes 44.1 Michée 7.14-7.15
6 Nakumbuka wimbo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu ikatafuta.Psaumes 4.4 Psaumes 42.8 Job 35.10 Ecclésiaste 1.16 Habakuk 3.17-3.18
7 Je! Bwana atatupa milele na milele? Hatatenda fadhili tena kabisa?Psaumes 85.1 Psaumes 85.5 Psaumes 89.38 Psaumes 79.5 Romains 11.1-11.2
8 Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote?Nombres 23.19 Romains 9.6 Esaïe 27.11 Nombres 14.34 Jérémie 15.18
9 Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?Esaïe 49.14-49.15 Esaïe 40.27 Romains 11.32 Esaïe 63.15 Psaumes 51.1
10 Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu.Psaumes 31.22 Job 42.3 Marc 9.24 Lamentations 3.18-3.23 Psaumes 116.11
11 Nitayakumbuka matendo ya Bwana; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.Psaumes 143.5 Psaumes 105.5 Esaïe 5.12 Psaumes 28.5 Psaumes 78.11
12 Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.Psaumes 145.4 Psaumes 143.5 Psaumes 105.2 Deutéronome 6.7 Luc 24.14-24.32
13 Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?Psaumes 73.17 Exode 15.11 Psaumes 63.2 Deutéronome 32.31 Psaumes 71.19
14 Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.Josué 9.9-9.10 Esaïe 51.9 Exode 15.11 Daniel 6.27 Psaumes 136.4
15 Kwa mkono wako umewakomboa watu wako, Wana wa Yakobo na Yusufu.Deutéronome 9.29 Exode 6.6 Psaumes 74.2 Esaïe 63.9 Genèse 48.3-48.20
16 Ee Mungu, yale maji yalikuona, Yale maji yalikuona, yakaogopa. Vilindi vya maji navyo vikatetemeka,Exode 14.21 Josué 3.15-3.16 Habakuk 3.8-3.10 Habakuk 3.15 Psaumes 114.3-114.6
17 Mawingu yakamwaga maji. Mbingu nazo zikatoa sauti, Mishale yako nayo ikatapakaa.Psaumes 18.14 Juges 5.4 Habakuk 3.11 Psaumes 68.33 Psaumes 68.8-68.9
18 Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli; Umeme uliuangaza ulimwengu. Nchi ilitetemeka na kutikisika;Psaumes 97.4 Apocalypse 18.1 Exode 19.16 Exode 19.18 Habakuk 3.4
19 Njia yako ilikuwa katika bahari. Na mapito yako yalikuwa katika maji makuu; Hatua zako hazikujulikana.Habakuk 3.15 Nahum 1.3-1.4 Exode 14.28 Néhémie 9.11 Psaumes 97.2
20 Uliwaongoza watu wako kama kundi, Kwa mkono wa Musa na Haruni.Exode 13.21 Psaumes 78.52 Esaïe 63.11-63.12 Psaumes 80.1 Exode 14.19

Cette Bible est dans le domaine public.