Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 63.1
Bible en Swahili de l’est


1 Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.Psaumes 84.2 Psaumes 143.6 Psaumes 42.1-42.2 Jérémie 31.1 Esaïe 41.18
2 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako.Psaumes 27.4 Psaumes 105.4 Psaumes 78.61 1 Chroniques 16.11 Psaumes 77.13-77.14
3 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.Psaumes 69.16 Philippiens 1.23 Psaumes 30.5 Psaumes 51.15 1 Corinthiens 6.20
4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.Psaumes 104.33 Psaumes 134.2 Psaumes 28.2 Habakuk 3.10 Psaumes 145.1-145.3
5 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.Psaumes 104.34 Psaumes 36.7-36.9 Psaumes 65.4 Psaumes 118.14-118.15 Esaïe 25.6
6 Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku.Psaumes 42.8 Cantique 5.2 Psaumes 119.147-119.148 Psaumes 149.5 Psaumes 77.4-77.6
7 Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.Psaumes 61.4 Psaumes 54.3-54.4 Psaumes 17.8 Psaumes 21.1 1 Samuel 17.37
8 Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza.Psaumes 18.35 Esaïe 41.10 Esaïe 42.1 Colossiens 1.29 2 Chroniques 31.21
9 Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu, Wataingia pande za nchi zilizo chini.Psaumes 55.15 Psaumes 40.14 Psaumes 9.17 Esaïe 14.15 Psaumes 86.13
10 Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, Watakuwa riziki za mbwa-mwitu.Jérémie 18.21 Ezéchiel 35.5 Ezéchiel 39.4 Cantique 2.15 Ezéchiel 39.17-39.20
11 Bali mfalme atamfurahia Mungu, Kila aapaye kwa Yeye atashangilia, Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.Esaïe 45.23 Deutéronome 6.13 Romains 3.19 Esaïe 65.16 Psaumes 21.1

Cette Bible est dans le domaine public.