1  Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake. 
Psaumes 37.7  Psaumes 33.20  Psaumes 37.39  Psaumes 121.2  Psaumes 123.2  
 2  Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana. 
Psaumes 18.2  Psaumes 59.17  Psaumes 62.6  2 Corinthiens 4.8-4.9  Psaumes 89.26  
 3  Hata lini mtamshambulia mtu, Mpate kumwua ninyi nyote pamoja? Kama ukuta unaoinama, Kama kitalu kilicho tayari kuanguka, 
Exode 16.28  Psaumes 21.11  Jérémie 4.14  Psaumes 140.2  Psaumes 38.12  
 4  Hufanya shauri kumwangusha tu katika cheo chake; Huufurahia uongo. Kwa kinywa chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani. 
Psaumes 28.3  Psaumes 55.21  Psaumes 5.9  Matthieu 26.3-26.4  Matthieu 22.15  
 5  Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya. Tumaini langu hutoka kwake. 
Psaumes 27.13-27.14  Michée 7.7  Psaumes 103.1-103.2  Philippiens 1.20  Psaumes 71.5  
 6  Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana. 
Psaumes 62.2  Psaumes 112.6  Psaumes 16.8  Proverbes 10.30  Proverbes 12.7  
 7  Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu. 
Jérémie 3.23  Psaumes 85.9  Esaïe 45.25  Psaumes 94.22  1 Corinthiens 1.30-1.31  
 8  Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. 
Lamentations 2.19  Philippiens 4.6  1 Samuel 1.15  Psaumes 142.2  Psaumes 42.4  
 9  Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili. 
Psaumes 39.5  Esaïe 40.17  Esaïe 40.15  Psaumes 39.11  2 Samuel 15.6  
 10  Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang’anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni. 
Esaïe 30.12  Psaumes 52.7  Job 20.29  1 Timothée 6.10  Esaïe 47.10  
 11  Mara moja amenena Mungu; Mara mbili nimeyasikia haya, Ya kuwa nguvu zina Mungu, 
Apocalypse 19.1  Jean 19.11  Matthieu 28.18  Psaumes 68.34-68.35  Esaïe 26.4  
 12  Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; Maana ndiwe umlipaye kila mtu Sawasawa na haki yake. 
Job 34.11  Psaumes 103.8  Matthieu 16.27  Daniel 9.9  1 Corinthiens 3.8