Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 62.10
Bible en Swahili de l’est


1 Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake.Psaumes 37.7 Psaumes 33.20 Psaumes 37.39 Psaumes 121.2 Psaumes 123.2
2 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana.Psaumes 18.2 Psaumes 59.17 Psaumes 62.6 2 Corinthiens 4.8-4.9 Psaumes 89.26
3 Hata lini mtamshambulia mtu, Mpate kumwua ninyi nyote pamoja? Kama ukuta unaoinama, Kama kitalu kilicho tayari kuanguka,Exode 16.28 Psaumes 21.11 Jérémie 4.14 Psaumes 140.2 Psaumes 38.12
4 Hufanya shauri kumwangusha tu katika cheo chake; Huufurahia uongo. Kwa kinywa chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani.Psaumes 28.3 Psaumes 55.21 Psaumes 5.9 Matthieu 26.3-26.4 Matthieu 22.15
5 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya. Tumaini langu hutoka kwake.Psaumes 27.13-27.14 Michée 7.7 Psaumes 103.1-103.2 Philippiens 1.20 Psaumes 71.5
6 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana.Psaumes 62.2 Psaumes 112.6 Psaumes 16.8 Proverbes 10.30 Proverbes 12.7
7 Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu.Jérémie 3.23 Psaumes 85.9 Esaïe 45.25 Psaumes 94.22 1 Corinthiens 1.30-1.31
8 Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.Lamentations 2.19 Philippiens 4.6 1 Samuel 1.15 Psaumes 142.2 Psaumes 42.4
9 Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.Psaumes 39.5 Esaïe 40.17 Esaïe 40.15 Psaumes 39.11 2 Samuel 15.6
10 Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang’anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.Esaïe 30.12 Psaumes 52.7 Job 20.29 1 Timothée 6.10 Esaïe 47.10
11 Mara moja amenena Mungu; Mara mbili nimeyasikia haya, Ya kuwa nguvu zina Mungu,Apocalypse 19.1 Jean 19.11 Matthieu 28.18 Psaumes 68.34-68.35 Esaïe 26.4
12 Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; Maana ndiwe umlipaye kila mtu Sawasawa na haki yake.Job 34.11 Psaumes 103.8 Matthieu 16.27 Daniel 9.9 1 Corinthiens 3.8

Cette Bible est dans le domaine public.