Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 62
Bible en Swahili de l’est


1 Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake. Psaumes 37.7 Psaumes 33.20 Psaumes 37.39 Luc 2.30-2.32 Esaïe 40.31
2 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana. Psaumes 18.2 Psaumes 59.17 2 Corinthiens 4.8-4.9 Psaumes 62.6 Psaumes 89.26
3 Hata lini mtamshambulia mtu, Mpate kumwua ninyi nyote pamoja? Kama ukuta unaoinama, Kama kitalu kilicho tayari kuanguka, Proverbes 1.22 Psaumes 82.2 Psaumes 4.2 Exode 16.28 Psaumes 21.11
4 Hufanya shauri kumwangusha tu katika cheo chake; Huufurahia uongo. Kwa kinywa chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani. Psaumes 28.3 Psaumes 55.21 Psaumes 5.9 Apocalypse 22.15 Luc 20.20
5 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya. Tumaini langu hutoka kwake. Michée 7.7 Psaumes 27.13-27.14 Psaumes 146.1 Psaumes 103.1-103.2 Philippiens 1.20
6 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana. Psaumes 62.2 Psaumes 112.6 Psaumes 16.8 Esaïe 45.17 Psaumes 18.31-18.32
7 Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu. Jérémie 3.23 Psaumes 85.9 Esaïe 45.25 Psaumes 94.22 Psaumes 95.1
8 Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. Philippiens 4.6 Lamentations 2.19 Psaumes 142.2 1 Samuel 1.15 Psaumes 42.4
9 Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili. Psaumes 39.5 Esaïe 40.15 Esaïe 40.17 Psaumes 39.11 1 Samuel 18.21-18.26
10 Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang’anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni. Esaïe 30.12 Psaumes 52.7 Deutéronome 6.10-6.12 Psaumes 91.14 Esaïe 28.15
11 Mara moja amenena Mungu; Mara mbili nimeyasikia haya, Ya kuwa nguvu zina Mungu, Apocalypse 19.1 Job 40.5 Jean 19.11 Matthieu 28.18 Psaumes 68.34-68.35
12 Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; Maana ndiwe umlipaye kila mtu Sawasawa na haki yake. Job 34.11 Psaumes 103.8 Matthieu 16.27 Psaumes 86.15 Romains 2.6

Cette Bible est dans le domaine public.