1  Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Umenifanyizia nafasi wakati wa shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu. 
Psaumes 18.18-18.19  Job 36.16  Jérémie 23.6  Exode 34.6-34.7  Psaumes 17.6  
 2  Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo? 
Osée 4.7  Psaumes 3.3  Psaumes 5.6  1 Samuel 12.21  Ephésiens 4.25  
 3  Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa; Bwana atasikia nimwitapo. 
2 Pierre 2.9  Psaumes 34.15  Psaumes 31.23  Psaumes 91.14-91.15  1 Pierre 2.9  
 4  Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia. 
Ephésiens 4.26  Psaumes 77.6  Psaumes 63.6  Psaumes 46.10  2 Corinthiens 13.5  
 5  Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana. 
Deutéronome 33.19  Psaumes 37.3  Psaumes 62.8  Psaumes 51.19  2 Samuel 15.12  
 6  Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema? Bwana, utuinulie nuru ya uso wako. 
Nombres 6.26  Psaumes 80.7  Psaumes 80.19  Psaumes 119.135  Psaumes 89.15  
 7  Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai. 
Esaïe 9.3  Psaumes 63.2-63.5  Actes 14.17  Psaumes 37.4  Cantique 1.4  
 8  Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama. 
Psaumes 3.5  Lévitique 25.18-25.19  Deutéronome 12.10  Lévitique 26.5  Psaumes 16.8-16.9